Liturujia ya Ekaristi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiini cha Misa katika seminari ya Asidonia-Jerez mwaka 2005 - wanaonekana altareni mapadri, mashemasi na watumishi wengine wakitambulikana kwa mavazi yao ya ibada yaliyo tofauti.

Liturujia ya Ekaristi ni sehemu ya pekee zaidi ya Misa.

Inafuata daima liturujia ya Neno na kuikamilisha kwa kumleta Yesu Kristo kati ya waamini wake kama chakula na kinywaji cha uzima kwa roho zao ili wapate nguvu na furaha kwa ajili ya kumfuata kwa kutekeleza Neno la Mungu lililotangazwa kwanza.

Mahali pake maalumu panaitwa altare (kutoka Kilatini) au madhabahu (kutoka Kiarabu), kwa sababu ukumbusho ulioachwa na Yesu katika karamu ya mwisho ni ukumbusho wa sadaka yake ya msalabani.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Ekaristi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.