Nenda kwa yaliyomo

Le Corbusier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Charles Le Corbusier (1964)

Charles-Édouard Jeanneret-Gris (alijulikana kwa jina la Le Corbusier; 6 Oktoba 188727 Agosti 1965) alikuwa msanifu majengo mashuhuri wa karne ya 20. Alisifiwa kwa vitabu vyake juu ya usanifu majengo na mpangilio wa miji. Alilenga hasa kuboresha makazi ya watu katika miji mikubwa iliyojaa watu wengi maskini. Alipenda pia kuchora picha na kutunga fanicha.

Le Corbusier alizaliwa Uswisi akachukua uraia wa Ufaransa katika miaka ya 1930.

Kama msanifu majengo alitaka kutumia nafasi ya teknolojia mpya ya saruji na chuma. Hapo alianzisha mafundisho yanayofuatwa na wajenzi hadi leo.

Nadharia ya ujenzi mpya[hariri | hariri chanzo]

Picha ya Le Corbusier kwenye pesa ya Uswisi.

Katika hoja tano kwa ujenzi wa kisasa alijumlisha madai yake:

1. Nguzo: Le Corbusier alitofautisha kati ya sehemu za jengo zinazoihitaji kubeba mzigo na kuta zisizobeba mzigo. Alitenga nguzo za saruji na chuma zinazobeba jengo kama mifupa. Nafasi kati ya hizi alifunga kwa kuta nyepesi. Kwa njia hiyo aliweza kupandisha jengo juu na kutumia nafasi chini yake; kuta zinaondoka katika uwiano wa ubichi wa udongo.

Aliwaza pia uwezekano wa kutenganisha paa na jengo lenyewe kwa kuiweka juu kama mwamvuli.

2. Paa bapa: Badala ya paa za kawaida zilizoinama kama kinga dhidi ya mvua Le Corbusier alitunga paa bapa pekee. Kwa njia hiyo alitaka kutumia eneo la paa kama ghorofa ya nyongeza au kwa ajili ya bustani ya juu katika mji mkubwa. Aliona tatizo la kupotea kwa ardhi katika miji mikubwa kwa hiyo alilenga kwa kuhifadhi eneo la bustani chini ya nyumba kwa kuipandisha juu ya nguzo au kuongeza sehemu ya bustani juu ya nyumba.

3. Uhuru wa mpangilio: Muundo wa nguzo ulimpa uhuru wa kupanga vyumba kufuatana na mapenzi yake au mapenzi ya watumiaji; tofauti na nyumba za awali ambako kuta zinazobeba mzigo zinapaswa kusimama juu ya ukuta wa ghorofa la chini.

4. Madirisha marefu: Nguzo za saruji zilimruhusu kupanga madirisha marefu kushinda ujenzi wa awali na kufungua ukuta wa nje kushinda mtindo wa zamani. Kwa njia hiyo aliweza kung'arisha vyumba vizuri zaidi. Kwa mtindo huu Le Corbusier alitunga madirisha ambayo vioo vyake vilisukumwa kando badala ya kufunguliwa kwa bawaba.

5. Uhuru wa kupanda uso wa nyumba: muundo wa nguzo za saruji uliimpa nafasi ya kuchaze na uso wa nyumba kwa sababu ukuta wa nje haukuhitaji kufuata masharti yoyote. Kwa kujenga ukuta wa usoni mbele ya nguzo aliweza kuipa nyumba uso bila kuuata mpangilio wa ndani, ghorofa n.k.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: