Leïla Marouane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Leïla Marouane ( alizaliwa mwaka 1960 katika nchini ya Tunisia) ni Mwandishi wa habari na Mwandishi wa riwaya zilizopokea tuzo mbalimbali katika fasihi ya Kifaransa.Jina lake kamili ni Leyla Zineb Mechentel.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Leyla alizaliwa nchini Tunisia mnamo mwaka 1960 katika mji wa Djerba, kisha familia yake ilihamia katika mji wa Biskra, familia yake iliishi hapo kwa muda hadi Leila alipofikisha umri wa miaka sita,Leila alihamia nchini Aljeria na baadae Ufaransa mwaka 1991 .[1] Alianza kuwa muandishi wa habari akiwa Aljeria akiandika makala na habari za kisiasa katika magazeti,alisoma katika chuo kikuu cha Paris 8 University hadi alipomaliza shahada yake ya uandishi,Kitabu chake cha La fille de la Casbah (katika Kiingereza The Daughter of the Kasbah) kilichapishwa na Éditions Julliard mwaka 1996 tangu wakati huo amechapisha vitabu mbalimbali vya riwaya , kitabu chake cha kwanza kutafsiriwa katikia Lugha ya Kiingereza kilitoka mwaka 1998 .[2]

Marouane ni muanzilishi wa La Boutique iliyoanzishwa mwaka 1996, ikiwa ni asasi iliyolenga kuendeleza na kukuza sanaa ya uandishi pamoja na kutangaza lugha ya Kifaransa na kingereza.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Algerian Author Leila Marouane On Religion, Politics and Writing". Africa Book Club (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2016-01-18. 
  2. ""The Sexual Life of an Islamist in Paris" by Leïla Marouane". Words Without Borders. Iliwekwa mnamo 2016-01-18. 
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leïla Marouane kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.