Lango:Kenya/Intro
Mandhari
Jamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi). Mji mkuu ni Nairobi.
Mji mkuu ni Nairobi. Idadi ya watu imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kufikia milioni 50. Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi maelfu ya wanyama pori wa kila aina.
Jina Kenya linatokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika, Kabla ya mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya liliitwa Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki, kwa hivyo hapakuwa na haja kutaja neno mlima uliporejelea mlima huo.