Kwanza (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwanza (Cuanza)
Mwendo wa mto Kwanza (Cuanza) katika Angola
Mwendo wa mto Kwanza (Cuanza) katika Angola
Chanzo karibu na Mumbue kwenye Nyanda za juu za Bié (Angola)
Mdomo Atlantiki
Nchi za beseni ya mto Angola
Urefu 965 km
Kimo cha chanzo 1,450 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 825 m³/s
Eneo la beseni (km²) 149,688 km²;

Kwanza (kwa Kireno: Cuanza, pia Coanza, Quanza au Kuanzani) ni mto katika Angola. Chanzo chake ni katika Nyanda za Juu za Bie ambako mito mingi mikubwa inaanza.

Jina la mto limekuwa pia jina la mikoa miwili ya Cuanza Norte (kaskazini kwa mto) na Cuanza Sul (kusini kwa mto).

Matawimto muhimu ni Kuiva, Luando na Lucala.

Mwendo wa mto[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mto unaelekea kaskazini halafu kaskazini-magharibi ikiwa mpaka kati ya mikoa ya Bie na Malange, baadaye kati ya mikoa ya Cuanza Sul na Malange, halafu kati ya mikoa ya Cuanza Sul na Bengo. Ikielekea magharibi inapita mkoa wa Cuanza Norte hadi kufikia Atlantiki kusini kwa Luanda, mji mkuu wa Angola.

Umuhimu wa kiuchumi[hariri | hariri chanzo]

Kwanza inatumika na meli kwa mwendo wa takriban km 250 kuanzia mdomo wake kungia barani. Kwa sababu hiyo ilikuwa pia njia ya Wareno ya kupeleleza Angola walipofika na kujenga utawala wao.

Kwanza inatumika kwa kutengeneza umeme kwa njia ya lambo la Capanda mkoani Malanje lililoanza kufanya kazi mwaka 2004.

Bado inatumika kama njia ya kusafirisha mizigo, pia maji yake humwagilia mashamba.

Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kwanza (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.