Kutangaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
mabango
Mabango ya matangazo huko Tokyo, Japani.

Kutangaza (kutoka kitenzi hicho hupatikana nomino tangazo) ni namna chama au kampuni inavyohamasisha watu wanunue bidhaa au huduma zao, lakini pia mawazo. Matangazo hujaribu kuvutia watu kwa kuonesha uzuri badala ya ubaya wa bidhaa zao.

Kwa kawaida huundwa na wakala wa matangazo kwa mdhamini, na kufanywa kwa vyombo vya habari. Matangazo hutangazwa kwenye runinga pia redio, magazeti, majarida na mabango mitaani na mijini.

Watangazaji hushawishi hisia kwa mbinu za kulenga watazamaji au wasikilizaji. Kwa mfano, kufanya mkate kuwa mtamu, unaweza kupakwa rangi za kumvutia mtazamaji.