Kujitoa kwa Joe Biden kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani
Mnamo Julai 21, 2024, Joe Biden, rais aliye madarakani wa Marekani, alitangaza kujiondoa katika uchaguzi wa urais wa Marekani 2024 kupitia taarifa aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii. Alimuidhinisha Makamu wa Rais Kamala Harris kama mgombea mbadala wake wa Chama cha Demokrasia katika uchaguzi huo.
Kuliibuka wasiwasi juu ya afya ya Biden wakati wa urais wake, haswa ukihusishwa umri na uwezo wake wa kutekeleza majukumu kwenye muhula wa pili. Licha ya matarajio tofauti ya watu, mnamo Aprili 25, 2023, Biden alitangaza kuwa atagombea tena kama rais katika uchaguzi wa 2024, na Harris angekuwa tena mgombea mwenza wake. Kampeni hiyo inarandana na kampeni ya miaka minne iliyopita, kampeni yake ya urais 2020 . Siku ya tangazo lake, kura ya maoni ya Gallup iligundua kuwa kiwango cha kukubalika kwa Biden kilikuwa asilimia 37, huku wengi wa wale waliohojiwa wakisema uchumi ndio wasiwasi wao mkubwa. Wakati wa kampeni yake, alinadi sera ya kiuchumi inayojulikana kama " Bidenomics " kufuatia janga la COVID-19 . Mara kwa mara alisema nia yake ya "kumaliza kazi" kama ujumbe wa mikutano yake ya kisiasa.
Wasiwasi kuhusu umri wa Biden ulifikia kiwango cha juu mnamo Juni 2024, kufuatia mdahalo kati ya Biden na mgombea wa Chama cha Republican Donald Trump . Utendaji wa Biden ulishutumiwa sana, na watoa maoni wakisema mara kwa mara alipoteza mwelekeo wa mawazo yake na kutoa majibu yasiyonyooka, alikuwa na hali ya kuyumbayumba, alizungumza kwa sauti ya kukoroma, na alishindwa kukumbuka takwimu au kutoa maoni yake mara kwa mara. Waandishi kadhaa wa magazeti walimtangaza Trump kuwa mshindi, na kura ya maoni ilionyesha kuwa wengi waliamini kuwa Trump alishinda. Mjadala huo ukiwa umeibua maswali kuhusu afya yake, Biden alikabiliwa na wito wa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho kutoka kwa Wanademokrasia wenzake na bodi za wahariri za vyombo kadhaa vikuu vya habari. Kufikia Julai 19, zaidi ya maafisa wakubwa 30 wa Chama cha Demokrasia, walikuwa wamemtaka ajiondoe.
Licha ya miito mingi ya kumtaka ajiondoe, Biden alisisitiza mara kwa mara kwamba atasalia kuwa mgombea. Hata hivyo, mnamo Julai 21, barua yenye saini yake iliwekwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa X iliyoarifu kujiondoa kwake kama mgombea, ikisema kwamba hiyo ni "kwa faida ya chama changu na nchi". Biden ni rais wa kwanza aliye madarakani anayestahili kuchaguliwa tena kuacha nia yake ya kuchaguliwa tena tangu Lyndon B. Johnson mwaka 1968, na rais wa kwanza katika historia ya Marekani kuchagua kutogombea tena baada ya kushinda kura za mchujo .
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Ugombea wa Biden
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Aprili 25, 2023, baada ya miezi kadhaa ya uvumi, Rais Joe Biden alithibitisha kuwa atagombea tena kama rais katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2024, na Makamu wa Rais Kamala Harris tena kama mgombea mwenza wake. Kampeni hiyo inarandana sana na kampeni yake ya urais 2020 . Siku ya tangazo lake, kura ya maoni ya Gallup iligundua kuwa kiwango cha uungwaji mkono kwa Biden kilikuwa asilimia 37, huku wengi wa wale waliohojiwa wakisema uchumi ndio wasiwasi wao mkubwa. Wakati wa kampeni yake, Biden alikuza ukuaji wa juu wa uchumi na ufufuaji kufuatia janga la UVIKO 19 (COVID 19) . Mara kwa mara alisema nia yake ya "kumaliza kazi" kama kauli mbiu yake kwenye mkutano wa kisiasa.
Kwenye kampeni yake, Biden alilipa kipaumbele suala la kulinda demokrasia ya Marekani,[1][2] ikiwa ni pamoja na kurejesha haki ya kitaifa ya utoaji mimba kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu ya shirikisho kufuta mwongozo wa Roe v. Wade.[3] Pia alidhamiria kuongeza fedha kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mipaka na utii wa sheria pamoja na maboresho ya mfumo wa kipolisi,[3][4] [5] Biden aliahidi kuunga mkono, kulinda na kutanua haki za wapenzi wa jinsi moja, LGBT[3] na mara zote alipigania kupitishwa Kwa sheria ya Uwekezaji kwenye Miundombinu na Ajira, Sheria ya Vikokotozi Kiduchu (Microchips) na Sayansi , na Sheria kifani ya Kupunguza Mfumuko wa Bei[6][7] pamoja na kuwekeza kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.[8]
Kuelekeza nguvu kwenye kuimarisha mahusiano na washirika wa Marekani ilikuwa lengo kuu la sera ya Biden ya mambo ya nje [9] na aliahidi kuendelea kuunga mkono Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi hiyo na kuibeba Israel kufuatia vita vyao na Hamas, akisema kuwa ni "muhimu" kwa maslahi ya usalama wa taifa la Marekani. Biden aliahidi kuendelea na juhudi za kukabiliana na uhalifu wa kutumia bunduki na kutetea Sheria ya Huduma za Bei Nafuu kufuatia maoni kutoka kwa Donald Trump alipoapa kuwa angefuta sheria hiyo. [10] [3] Biden alipendekeza kuongeza ushuru kwa matajiri kupitia mpango wa "ukomo wa chini wa kodi ya mapato ya mabilionea" ili kupunguza nakisi na kufadhili huduma za kijamii kwa watu wa hali ya chinii. [11] [3]
Sera ya mambo ya biashara ya Biden ilielezewa kuwa ni inayokataa sera ya jadi ya uchumi wa kiliberali mamboleo na Makubaliano ya Washington ambayo yalisababisha kuzoroteshwa kwa utengenezaji wa bidhaa na hivyo kusababisha kuongezeka kwa ukinzani wa nguvu ya umma . Biden alipendekeza na kupitisha ushuru unaolengwa dhidi ya viwanda vya kimkakati vya China ili kulinda ajira za sekta ya viwanda na kukabiliana na mipango ya kiteknolojia na kijeshi ya China. Biden hakuwa kwenye sanduku la uchaguzi wa Januari 23, New Hampshire, lakini alishinda katika kampeni ya kura ya moja kwa moja kwa 63.8% ya kura. Alikuwa akitaka Carolina Kusini iwe ya kwanza katika mchujo wa kwanza, na alishinda jimbo hilo mnamo Februari 3 kwa 96.2% ya kura. Biden alipata 89.3% ya kura huko Nevada na 81.1% ya kura huko Michigan, akiwaacha mbali wapinzani wake katika kila jimbo, mtawalia. Mnamo Machi 5 ("Jumanne Kuu"), alishinda kura 15 kati ya 16, na kupata 80% au zaidi ya kura katika majimbo 13 kati ya 15. [12] Mnamo Machi 12, alifikia zaidi ya wajumbe 1,968 waliohitajika kushinda uteuzi wa Chama cha Kidemokrasia, na kuwa mteule aliyepita kabla mchakato kuisha.
Umri wa Biden na afya yake
[hariri | hariri chanzo]Katika kuapishwa kwake, Biden alikula kiapo cha ofisi akiwa na umri wa miaka 78, na kumfanya kuwa mtu mzee zaidi kushika wadhifa huo. [13] Biden alikuwa mzee alipochukua madaraka kuliko rais mwingine yeyote alipokuwa akiondoka madarakani. Wasiwasi juu ya afya ya Biden uliibuka wakati wa urais wake, haswa kuhusu umri wake na uwezo wa kuumudu muhula wa pili. Kwenye ripoti katika Jarida la Active Aging, madaktari walibainisha kuwa alikuwa na "wasifu wa kipekee wa kiafya" kulingana na umri wake, na tathmini ya kimatibabu iliyofanywa na daktari Kevin O'Connor ilithibitisha utete wake wa kimwili. [14] Dan Zak wa ' gazeti la Washington Post alielezea serikali ya Marekani kama serikali ya wazee wakati wa kuapishwa kwa Biden.
Mnamo Julai 2024, The New York Times liliripoti kwamba Kevin Cannard, daktari wa neva kutoka Kituo cha Kitaifa cha Kijeshi cha Walter Reed aliyebobea katika magonjwa yahusuyo kujongea kama ugonjwa wa Parkinson, alitembelea Ikulu ya White House mara nane ndani ya miezi minane iliyopita, ukijumuisha kukutana kwake na daktari wa Biden. [15] Ripoti hiyo ilizua utata kwani O'Connor aliikanusha, akitoa mfano wa kuonana kwa Cannard wakati wa utawala wa Barack Obama na wafanyakazi ndani ya Ikulu ya White House ambao walikuwa na matatizo ya neva. [16]
Mdahalao na Trump
[hariri | hariri chanzo]Biden alikabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya mjadala mbashara wa televisheni dhidi ya Trump mnamo Juni 27, 2024, huku Wanademokratiki wengi wakikosoa utendaji, ambapo Biden alikuwa na mwonekano wa kuyumbayumba na alizungumza kwa sauti ya mikwaruzo. [17] Kufuatia utendaji wa Biden katika mdahalo huo, Wanademokratiki wengi walimtaka ajiondoe kwenye kinyang'anyiro hicho, na kusababisha msukosuko wa kisiasa ndani ya chama hicho kiasi kwamba vyombo vya habari waliuita "mgogoro wa Biden".
Matokeo ya mdahalo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Julai 17, ABC News iliripoti kwamba kiongozi wa wachache wa Bungeni Hakeem Jeffries na kiongozi wa wengi wa Seneti Chuck Schumer walikutana na Biden mnamo Julai 12 na 13, mtawalia, na walikuwa wameelezea wasiwasi wao kwa Biden kuhusu kushindwa Kwa Chama cha Kidemokrasia katika Congress. [18] Biden aliripotiwa kumwambia Schumer kwamba alihitaji wiki moja kufanya uamuzi. [19] Jeffrey Katzenberg, mwenyekiti mwenza wa kampeni, aliripotiwa kumuonya Biden mnamo Julai 17 kwamba wafadhili walikuwa wakisitisha ufadhili wa kampeni yake, ingawa Katzenberg hakupendezwa na maudhui ya majadiliano yao. [20]
Jioni hiyo, Biden alipimwa na kukutwa na maambukizi ya UVIKO 19 (COVID-19) . [21] Allionekana na dalili kidogo, ikiwa ni pamoja na kikohozi, kutoa kamasi, na " dalili nyinginezo za maradhi ". Hali kadhalika, taswira zake kwenye picha zilizomuonesha akiwa dhaifu wakati akishuka kwenye Air Force One akienda kujitenga katika makazi yake huko Rehoboth Beach, Delaware, zilichochea uvumi zaidi juu ya afya yake. Gazeti la New York Times liliripoti kwamba Biden alikuwa "mwenye kukubali zaidi" kuondoa uteuzi wake. [22] Katika mazungumzo ya simu, spika wa zamani wa Ikulu Nancy Pelosi alimwambia Biden alikuwa na matarajio kuwa [Biden] asingegombe. [23] Mnamo Julai 18, Axios iliripoti kwamba Wanademokratiki waliamini kuwa Biden angejitoa kwenye uchaguzi, wakirejea shinikizo kutoka kwa Jeffries na Schumer, upigaji kura wa ndani, na ukosoaji. [24] Gazeti la New York Times liliripoti siku hiyo kwamba Biden alikuwa akifikiria kuhusu kujiondoa. Kufikia jioni ya Julai 20, Biden alianza kupanga juu ya kujitoa kwenye kinyang'anyiro kwa kuwashirikisha washauri wa karibu, na alifikia uamuzi wa mwisho asubuhi ya Julai 21.
Kabla ya kujitoa kwa Biden, neno Joever ( /dʒ oʊ . v ər / JOH -vər ), umbi-neno lenye maana ya Joe na kwisha, lilitumiwa na wakosoaji na vyombo vya habari kuelezea hali ya kampeni ya Biden. Neno hili lilitokana na chapisho la mwaka 2020 la 4chan lililomkejeli Biden alipodhaniwa hatoweza kushinda uchaguzi wa 2020, na kwa haraka likawa meme [kitu cha mzaha kisambaacho kwa kasi] maarufu ya mtandaoni, haswa Kwenye Twitter . Meme ya Joever ilipata umaarufu mkubwa mnamo 2024 huku wasiwasi juu ya siha na afya yake zikiongezeka. [25]
Miitikio ya kampeni
[hariri | hariri chanzo]Mkakati
[hariri | hariri chanzo]Kampeni ya Biden ilitumia mkakati wa kupunguza nguvu za maoni ya kutaka kujiondoa kwa Biden hadi alipoteuliwa rasmi kupitia kura iliyodhaniwa kuwa ya kuwaita kwa majina wapiga kura, kabla ya Kongamano la Kitaifa la Wanademokratiki, ambalo liliisha ndani ya saa moja. [26]
Sera
[hariri | hariri chanzo]Kujibu lawama zilizofuatia mdahalao wake na Trump, Biden alitangaza sera kadhaa za kimaendeleo, [27] ikiwa ni pamoja na mageuzi ndani ya Mahakama ya Juu ili kuweka ukomo wa muhula na kanuni za maadili, marekebisho ya katiba ya kuanzisha mamlaka ya mwendesha mashtaka juu ya matendo ya rais, marufuku ya kitaifa ya silaha za mashambulizi, na. kupunguza ongezeko la kodi za pango. [28]
Kujitoa
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Julai 21, akaunti rasmi ya Rais Joe Biden kaika mtandao wa X, ilichapisha barua iliyotangaza kujiondoa kwake. Katika barua hiyo, aliandika, " ... ingawa imekuwa nia yangu kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiuzulu na kuelekeza nguvu zangu kipekee katika kutimiza wajibu wangu kama Rais wa nchi katika muda uliosalia wa kipindi changu." Baadae, siku hiyo hiyo, chapisho kwenye akaunti hiyo hiyo lilimuidhinisha Harris, makamu wa rais tangu 2021, kama mbadala wake katika kinyang'anyiro cha urais. [29]
Mbadala wa mgombea
[hariri | hariri chanzo]Wajumbe wala kiapo wa Biden walibaki huru kufuatia kujiuzulu kwake kutoka kwenye kinyang'anyiro hicho. Sasa, mgombea atakayepata saini 300 kutoka kwa wajumbe atatokea kwenye orodha ya wagombea urais. Ni lazima mgombea apate kura nyingi za wajumbe katika kongamano ili awe mteuliwa; ikiwa hakuna mgombeaji aliyepata kura nyingi hapo awali, wajumbe wakuu 700 zaidi wanaruhusiwa kumpigia kura mgombeaji. [30] Wajumbe wote karibu 3,800 waliojitolea hapo awali kwa Biden hawatofungwa. Yaani, hata kama Biden amemwidhinisha Harris, sheria za Kamati ya Kitaifa ya Wademokratiki hazihitaji wajumbe hawa kufuata mapendekezo yake na kumuunga mkono mrithi wake aliyechaguliwa. [31]
Katika uchunguzi juu ya wajumbe uliofanywa na Associated Press mnamo Julai 22, 2024, Kamala Harris alikua mgombeaji mpya baada ya kupata ahadi kutoka kwa zaidi ya nusu ya wajumbe. [32]
Miitikio ya kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Chama cha Kidemokrasia
[hariri | hariri chanzo]Marais wa zamani Bill Clinton na Barack Obama walisifu kazi ya Biden kama rais, ambapo Obama akiandika kuwa "Joe Biden amekuwa mmoja wa marais wa Marekani walioleta tija" na kwamba Biden "hangefanya uamuzi huu isipokuwa kwa kuamini kuwa ni sahihi kwa Marekani." [33] Wanademokratiki wengi walisifu uamuzi wa Biden kuwa "hakuwa mbinafsi". Watu hao ni kama vile Mbunge wa South Carolina Jim Clyburn, mshauri wa Obama David Axelrod, na Mbunge wa Ohio Greg Landsman, huku Kiongozi wa Wengi katika Seneti Chuck Schumer akiandika kwamba kwa mara nyingine Biden "ameiweka nchi yake, chama chake., na mustakabali wetu mbele" na kuiweka nafsi yake nyuma. [34] Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na mgombea urais Hillary Clinton alifanya vivyo hivyo na kumuidhinisha Harris. [35]
Kampeni ya Trump
[hariri | hariri chanzo]Kufuatia tangazo la kujiondoa kwa Biden, Trump alitoa taarifa kwenye mtandao wake wa kijamii, Truth Social, akisema kuwa mpinzani wake wa zamani "hakufaa kugombea Urais, na kwa hakika hafai kuhudumu", akimuelezea kama "Rais wa ovyo kuliko wote walopata kutokea katika historia ya nchi yetu". [36] Kampeni ya kuchaguliwa tena kwa Trump imetayarisha ripoti za utafiti wa upinzani kuhusu Kamala Harris na gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro . Kampeni ilinuia kutoa ujumbe wa kumkosoa vikali Harris katika Kongamano la Kitaifa la Republican, lakini baadae ikaamua kuitupilia mbali nia yake hiyo.
Mwitikio wa kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Mataifa mbalimbali yamekuwa na maoni juu ya kinachoendelea Marekani. Mataifa hayo ni pamoja na Australia[37] Brazil, Canada, China, Jamhuri ya Czech, Ujerumani, Ireland, Israel, New Zealand, Norway, Philippines, and others.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Epstein, Reid J.. "Biden Condemns Trump as Dire Threat to Democracy in a Blistering Speech", New York Times, January 5, 2024.
- ↑ "Transcript: Biden's first campaign speech of the 2024 election year", Associated Press, January 5, 2024.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Megerian, Chris. "Joe Biden wants to complete his goals on civil rights, taxes, and social services if he's reelected", Associated Press, November 12, 2023.
- ↑ Nichols, Hans. "Biden pledges to campaign "every day" on Trump's border meddling", February 6, 2024.
- ↑ Kanno-Youngs, Zolan. "Many of Biden's Goals on Police Reform Are Still Incomplete", New York Times, February 8, 2023.
- ↑ Dennis, Brady. "As Congress funds high-tech climate solutions, it also bets on a low-tech one: Nature", The Washington Post, August 14, 2022.
- ↑ Kaufman, Anna. "What is the Inflation Reduction Act 2022? Answering your common questions about the bill.", September 23, 2022.
- ↑ Sasso, Michael. "What Is Bidenomics? It Depends If You're a Democrat or Republican", Bloomberg News, January 11, 2024.
- ↑ Madhani, Aamer. "Biden declares 'America is back' in welcome words to allies", Associated Press, February 19, 2021.
- ↑ Reid J. Epstein. "Biden Campaign Aims to Weaponize Trump's Threat to Obamacare", New York Times, November 27, 2023.
- ↑ Hussein, Fatima. "EXPLAINER: How would billionaire income tax work?", Associated Press, March 29, 2022.
- ↑ "2024 U.S. Election – Latest News and Updates on Presidential and State Races". Yahoo!. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 20, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Dovere, Edward-Isaac (Januari 21, 2021). "The Biden Generation's Last Chance". The Atlantic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 19, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Sadeghi, McKenzie (Januari 5, 2021). "False news report indicates Biden plans to step down as president-elect". USA Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 18, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Baumgaertner, Emily (Julai 8, 2024). "Parkinson's Expert Visited the White House Eight Times in Eight Months". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 18, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The Biden-Parkinson's mini-controversy, explained", The Washington Post, July 9, 2024.
- ↑ Korecki, Natasha (Juni 28, 2024). "'Babbling' and 'hoarse': Biden's debate performance sends Democrats into a panic". NBC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 28, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Schumer privately urged Biden to step aside in 2024 election: Sources", ABC News, July 17, 2024. (en)
- ↑ "Inside the Weekend When Biden Decided to Withdraw", The New York Times, July 21, 2024.
- ↑ "Donors' cash is drying up, Katzenberg warns Biden in private meeting", Semafor.
- ↑ Shear, Michael (Julai 17, 2024). "Biden Tests Positive for Covid". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 19, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hulse, Carl (Julai 18, 2024). "Biden Called 'More Receptive' to Hearing Pleas to Step Aside". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 18, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hulse, Carl (Julai 18, 2024). "Pelosi has told Biden she is pessimistic about his chances of beating Trump". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 19, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ VandeHei, Jim (Julai 18, 2024). "Top Dems now believe Biden will exit". Axios. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Placido, Dani Di. "Joe Biden's 'It's Joever' Meme, Explained". Forbes. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 22, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nagourney, Adam (Julai 10, 2024). "A Late Play by the Biden Campaign: Running Out the Clock". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 18, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Thompson, Alex (Julai 17, 2024). "Biden's rescue operation: Leap left to survive". Axios. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Narea, Nicole (Julai 18, 2024). "Biden is betting on impossible promises to progressives". Vox. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 22, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 20, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Shear, Michael (Julai 21, 2024). "Biden Drops Out of Presidential Race, Endorses Harris". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 21, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kamisar, Ben (Juni 27, 2024). "Democrats are talking about replacing Joe Biden. That wouldn't be so easy". NBC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 28, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Montellaro, Zach. "What happens next now that Biden has dropped out?", Politico, July 21, 2024.
- ↑ "Harris Crosses Delegate Threshold in Sign Nomination Is Hers". Bloomberg News. Julai 22, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 22, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Obama, Barack (Julai 21, 2024). "Bill and Hillary Clinton Endorse Kamala Harris". Medium. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 21, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Groves, Stephen (Julai 21, 2024). "Democrats hail Biden's decision to not seek reelection as selfless. Republicans urge him to resign". Associated Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 21, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rumpf, Sarah (Julai 21, 2024). "My Statement on President Biden's Announcement". Mediaite. Iliwekwa mnamo Julai 21, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "'Worst president': Donald Trump reacts to President Joe Biden dropping out of 2024 election", July 21, 2024.
- ↑ "Biden withdraws from campaign: How foreign leaders are reacting". Reuters. Julai 22, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 22, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kujitoa kwa Joe Biden kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |