Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1968

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1968 ulikuwa wa 46 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 5 Novemba. Upande wa "Republican Party", mgombea Richard Nixon (pamoja na kaimu wake Spiro Agnew) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party" Hubert Humphrey (pamoja na kaimu wake Edmund Muskie) na mgombea wa "American Independent Party" George Wallace (pamoja na kaimu wake Curtis LeMay).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Nixon akapata kura 301, Humphrey 191 na Wallace 46 (pamoja na kura moja wa mchaguzi kutoka North Carolina aliyempigia kura Wallace badala ya Nixon). Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.