Hubert Humphrey
Mandhari
Hubert Horatio Humphrey Jr. (27 Mei, 1911 – 13 Januari, 1978) alikuwa mwanasiasa wa Marekani. Kuanzia mwaka wa 1949 hadi 1964 alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Minnesota. Halafu alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais Lyndon B. Johnson kuanzia mwaka wa 1965 hadi 1969. Mwaka wa 1968 aligombea urais yeye mwenyewe lakini akashindwa na Rais Richard Nixon. Kuanzia 1971 hadi kifo chake 1978 akawa seneta wa Minnesota tena.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hubert Humphrey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |