Spiro Agnew

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spiro Agnew, Kaimu Rais wa Marekani

Spiro Theodore Agnew (9 Novemba, 191817 Septemba, 1996) alikuwa mwanasiasa wa Marekani. Kuanzia mwaka wa 1967 hadi 1969 alikuwa gavana wa jimbo la Maryland. Halafu alikuwa Kaimu Rais wa Marekani chini ya Rais Richard Nixon kuanzia mwaka wa 1969 hadi 1973. Alishtakiwa na kugunduliwa kuwa na hatia ya rushwa, akajiuzulu tarehe 10 Oktoba 1973. Rais Nixon akamchagua Gerald Ford amfuate Agnew kama Kaimu Rais.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Spiro Agnew kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.