Kituo egeshi

Tarakilishi bapa juu ya kituo egeshi.
Katika utarakilishi, kituo egeshi (kwa Kiingereza: docking station, port replicator (hub) au dock) ni kitu kinachotumika ili kuunganisha tarakilishi mpakato na kipembezo kingine. Lakini, leo kituo egeshi kinatumika kwa vifaa vingine vingi kama simu au kipanya. Kwa mfano, kifaa cha mchezo video kinachoitwa Switch na Nintendo kinatumia kituo egeshi ili kuchaji umeme Switch na kuonyesha kiwambo cha Switch katika televisheni.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Kahigi, K. K. (2007). Ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili Sanifu. Kioo cha Lugha, 5(1).