Kiore
Kiore ni kata ya Wilaya ya Tarime katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31425. Kata ya Kiore iligawanywa toka kata ya zamani ya Nyandoto.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 12,265 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,020 waishio humo [2].
Jina linatokana na mlima Kiore uliopo kati ya vijiji vya Nyagisya na Kewamamba. Mkaazi mkongwe wa Kitongoji cha Kiore-Nyagisya, Anthony Roche (91) alisema wakaazi wa Kiore ni Wakuria jamii ya Wasweta waliosambaratishwa na mabomu ya Wajerumani kutoka ngome yao iliyojulikana kama Kwigori wakati wa ukoloni. Baada ya shambulio la mabomu walisambaa kuzingira mlima Kiore.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Tarime Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania |
||||
---|---|---|---|---|
Binagi * Bumera * Ganyange * Gorong'a * Gwitiryo * Itiryo * Kemambo * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Kwihancha * Manga * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nyakonga * Nyamwaga * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Regicheri * Sirari * Susuni
|