Kikunde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kikunde ni jina la kata ya Wilaya ya Kilindi katika Mkoa wa Tanga , Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 10,468 [1] waishio humo.

Wakazi wake ni wakulima na wafugaji wakiwa Wakaguru, Wanguu na Wamasai. Mazao ya chakula ni mahindi, maharage, mihogo na mbaazi. Kata hii ni maarufu kwa matunda aina ya maembe.

Kata ya Kikunde inajumuisha vijiji vya Kikunde, Tunguli, Mafulila, Ludewa, Mjimpya na Lusane. Kata ya Kikunde ya awali imegawanywa na kufanya kuwa kata mbili tofauti, ambapo kata mpya ya Tunguli imeanzishwa, mnamo mwaka 2011, na kata hiyo ina vijiji vifuatavyo, Tunguli, Manyinga, Mtolo, Msamvu, na Lusane.

Kata ya Tunguli ina shule za msingi nne, ambazo ni, Mjimpya, Lusane, Manyinga, na Tunguli. Pia ina shule moja ya sekondari ya Tunguli, lakini bado jitihada zinaendelea ili kuongeza shule ya pili..

Kituo cha afya cha Tunguli kinachomilikiwa na kanisa la Anglikana kinahudumia kata nzima na nyingine.Shule za msingi zipo kila kijiji na Kikunde ipo shule ya sekondari.

Wananchi wa kata hii hawana zao maalum za biashara isipokuwa maharagwe na maembe wakati wa msimu. Kwa wafugaji huuza mifugo yao katika mnada wa kila mwezi mara moja uliopo Kikunde.

Madini ya dhahabu ni utajiri uliogunduliwa hivi karibuni katika vijiji vya Mafulila na Tunguli. Kata hii ina misitu ya hifadhi na miti ya mbao.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Tanga - Kilindi DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-17.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kikunde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Kata za Wilaya ya Kilindi - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Jaila | Kibirashi | Kikunde | Kilindi | Kilwa | Kimbe | Kisangasa | Kwediboma | Kwekivu | Lwande | Mabalanga | Masagulu | Mkindi | Msanja | Mvungwe | Negero | Pagwi | Saunyi | Songe | Tunguli