Kijogoo-shamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kijogoo-shamba
Kijogoo-shamba utosi-mweusi
Kijogoo-shamba utosi-mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Eurylaimoidea (Ndege kama vijogoo-shamba)
Familia: Eurylaimidae (Ndege walio na mnasaba na vijogoo-shamba)
Jenasi: Calyptomena Raffles, 1822

Corydon Lesson, 1828
Cymbirhynchus Vigors, 1830
Eurylaimus Horsfield, 1821
Psarisomus Swainson, 1837
Pseudocalyptomena Rothschild, 1909
Serilophus Swainson, 1837
Smithornis Bonaparte, 1850

Vijogoo-shamba au bandabanda ni ndege wa familia Eurylaimidae. Wana domo pana na spishi nyingi zina rangi kali lakini zile za Afrika ni kahawia na nyeupe zenye michirizi myeusi isipokuwa kijogoo-shamba kijani ambaye ana rangi ya majani. Ndege hawa wanatokea misitu mizito. Hula matunda na hukamata wadudu kwa namna ya shore au chechele. Hupenda kuwa kwa makundi ya hadi kufikia ndege 20. Tago la vijogoo-shamba ni mjengo mkubwa (mpaka nusu mita) unaofungika na wenye mwingilio kwa upande wake. Limefumika kwa vitawi, manyasi na majani na kufunikika kwa tando za buibui, vigoga na kuvumwani. Jike huyataga mayai 1-3.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]