Kijogoo-shamba
Kijogoo-shamba | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kijogoo-shamba utosi-mweusi
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 2, spishi 6 + 1 kutoka familia nyingine:
|
Vijogoo-shamba au bandabanda ni ndege wa familia Calyptomenidae. Zamani ndege hawa waliainishwa katika familia Eurylaimidae lakini siku hizi inabaki spishi moja tu ndani yake, kijogoo-shamba kijani.
Wana domo pana na spishi za Asia pamoja na kijogoo-shamba kijani zina rangi ya majani lakini spishi nyingine za Afrika ni kahawia na nyeupe zenye michirizi myeusi. Ndege hawa wanatokea misitu mizito. Hula matunda na hukamata wadudu kwa namna ya shore au chechele. Hupenda kuwa kwa makundi ya hadi kufikia ndege 20. Tago la vijogoo-shamba ni mjengo mkubwa (mpaka nusu mita) unaofungika na wenye mwingilio kwa upande wake. Limefumika kwa vitawi, manyasi na majani na kufunikika kwa tando za buibui, vigoga na kuvumwani. Jike huyataga mayai 1-3.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Pseudocalyptomena graueri, Kijogoo-shamba Kijani (Grauer's au African Green Broadbill)
- Smithornis capensis, Kijogoo-shamba Utosi-mweusi (African Broadbill)
- Smithornis rufolateralis, Kijogoo-shamba Mabega-mekundu ( Rufous-sided Broadbill)
- Smithornis sharpei, Kijogoo-shamba Kichwa-kijivu (Grey-headed Broadbill)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Calyptomena hosii (Hose's Broadbill)
- Calyptomena viridis (Green Broadbill)
- Calyptomena whiteheadi (Whitehead's Broadbill)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kijogoo-shamba mabega-mekundu
-
Green broadbill