Kijiji Kisicho na Makaburi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kijiji Kisicho na Makaburi [1] ni riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na mtunzi wa riwaya Dickson Mtalaze.

Inazungumzia mkasa katika kijiji kimoja katika mkoa wa Simiyu ambacho wananchi wake walikuwa wanaishi bila ya kuwa na makaburi, hali ambayo iliwashangaza wengi walioingia katika kijiji hicho kwa mara ya kwanza.

Ni simulizi inayomhusisha mwalimu Dickson ambaye anapata ajira ya serikali kwa mara ya kwanza baada ya kuishi katika kijiji chake cha Kibakwe, mkoa wa Dodoma bila ya kuwa na ajira ya fani aliyosomea.

Dick anapata kazi ya ualimu katika kijiji cha maajabu ambacho anajikuta akiingia katika sakata zito la kupambana na uchawi mzito baada ya kumuadhibu mwanafunzi mmoja wa kike.

Ni kitabu ambacho simulizi yake inafanana kabisa na visa vya kuogopesha vinavyodaiwa kutokea katika kijiji cha Gambosi.

Kitabu hiki kilizinduliwa na Richard S Mabala ambaye ni mwandishi wa vitabu mbalimbali vinavyotumika katika shule za Sekondari nchini pia Richard Mabala ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kijiji Kisicho na Makaburi kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.