Kenya People's Union

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kenya People's Union ni Chama cha Kisiasa nchini Kenya kilichoongozwa na Oginga Odinga ambacho baadaye kilipigwa marufuku mnamo 1969.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Machi 1966, mzozo ulitokea katika mkutano wa chama tawala KANU uliyofanya mlengo wa kushoto wa chama ukiacha chama hicho na kuanzisha KPU[1]. KANU ilibadilisha sheria za uchaguzi kulazimisha wabunge waliyejiunga na KPU kutetea viti vyao katika uchaguzi mdogo. KPU iliweza kushinda hasa kwa Waluo Mkoani Nyanza pekee, huku waliyesimama kwingine wakishindwa na wanasiasa kutoka chama cha KANU ambacho wakati huo kilikuwa kikitawalwa na wanasiasa Wakikuyu [2]. Mwisho wa Chama hiki uliwadia wakati wa Ufunguzi wa Hospitali ya New Nyanza mnamo 25 Oktoba 1969. Wakati huo rais Jomo Kenyatta hakupendezwa na ufunguzi wa hospitali hiyo kwa vile ilijengwa na fedha za Soviet na ilionekana kama mradi wa Odinga. Hata hivyo Kenyatta aliongoza sherehe za ufunguzi wake ili kuimarisha umaarufu wake Mkoani Nyanza. Wajaluo walijulikana kuwa wenye hasira mno kwa kawaida, hasa kwa serikali tangu mauaji ya Tom Mboya miezi michache iliyotangulia, huku vidole vingi vikimwelekea Kenyatta. Maandamano yalianzishwa wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wakati wafuazi wa KPU waliushanbulia msafara wa rais. Zaidi ya watu kumi waliuawa wakati walinzi wa Kenyatta walifunguaufyatuaji wa risasi dhidi ya waandamanaji hao. Odinga na maafisa wengine wa chama cha KPU walititiwa nguvuni siku mbili baada ya tukio hilo. KPU kilifutiliwa mbali mnamo 30 Oktoba 1969, huku Kenya ikibakia na Chama Kimoja[3].

Wanasiasa wa KPU[hariri | hariri chanzo]

Wafuatao ni wanasiasa waliojiunga na KPU. ‘’Katika mabano ni jimbo la uchaguzi walilowakilisha’’ [4].[3]:

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bethwell A. Ogot, William Robert Ochieng': Decolonization and independence in Kenya. 1995
  2. Abner Cohen: Urban Ethnicity. Routledge, 2004. ISBN 0-415-32982-5
  3. 3.0 3.1 Daily Nation, 23 Oktoba 2009: The incident that transformed Kenya into a de facto one-party state Archived 1 Februari 2018 at the Wayback Machine.
  4. Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.