Kenya Commercial Bank (Uganda)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kenya Commercial Bank (Uganda)
Ilipoanzishwa2007
Makao MakuuCommercial Plaza, Kampala Road, Kampala, Uganda Uganda
Tovutihttp://www.kcbbankgroup.com/ug

Kenya Commercial Bank (Uganda) (KCB), pia hujulikana kama KCB Uganda ni benki ya biashara nchini Uganda. Inalenga kutimiza mahitaji ya kibenki ya watu binafsi na makampuni.

Kundi la Kenya Commercial Bank[hariri | hariri chanzo]

Kenya Commercial Bank (Uganda) ni mwanachama wa kampuni za KCB Group, ambazo ni:

KCB Group ndio kundi kubwa zaidi ya huduma za kifedha katika Afrika Mashariki, pamoja na wigo wa mali zaidi ya juu US $ 2.5. Kotoka Julai 2009, KCB Group ina mtandao wa mkubwa zaidi wa matawi ya benki likijumuisha zaidi ya matawi 180 nchini Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Novemba 2007, tawi la kwanza la KCB Uganda lilifunguliwa Kampala nchini Uganda, baada ya kupewa leseni na Benki ya Uganda. Tangu wakati huo, KCB Uganda imefungua matawi zaidi ya kumi na tatu nchini Uganda. KCB Group inamiliki 100% ya KCB Uganda. Hisa ya KCB Group ni hufanyiwa biashara katika masoko ya hisa ya Afrika Mashariki yafwatayo chini ya kiashirio "KCB":[1]

Mtandao wa matawi[hariri | hariri chanzo]

KCB Uganda ina mtandao wa matawi kumi na nne mashariki, kaskazini na magharibi mwa Uganda. Miongoni mwa maeneo ambako benki hili lina matawi ni:[2][3]

  1. Tawi la Arua - Arua
  2. Tawi la Gulu - Gulu
  3. Tawi la Lira - Lira
  4. Tawi la Mbale - Mbale
  5. Tawi Kuu - Barabara la Kampala, Kampala
  6. Tawi la Ben Kiwanuka - Barabara la Ben Kiwanuka, Kampala
  7. Tawi la Barabara la Luwuum - Barabara la Luwuum, Kampala
  8. Tawi la Ndeeba - Ndeeba, Kampala
  9. Tawi la Hoima - Hoima
  10. Tawi la Fort Portal - Fort Portal
  11. Tawi la Mbarara - Mbarara
  12. Tawi la Kabale - Kabale
  13. Tawi la Masaka - Masaka
  14. Tawi la Jinja - Jinja

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]