Kenny Thomas
Kenny Thomas | |
---|---|
Jina Kamili | Kenny Thomas |
Jina la kisanii | Kenny Thomas |
Nchi | Uingereza |
Alizaliwa | 12 Septemba 1968 |
Aina ya muziki | Soul, R&B |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Miaka ya kazi | 1988 - hadi leo |
Kenny Thomas (alizaliwa Islington, London, 12 Septemba 1968) ni mwimbaji kutoka Uingereza ambaye alikuwa na kazi nzuri katika miaka ya 1990, akiingiza nyimbo nane kwenye chati za UK top 40.[1][2]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Thomas alikulia Hillside Estate, Stamford Hill na alihudhuria shule ya Kardinali Pole Roman Catholic huko Hackney. Aliwahi kuwa bondia na fundi kwenye kampuni ya BT technician kabla ya kuanza kazi kama mwimbaji.
Sasa anaishi Costessey karibu na Norwich.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mafanikio ya Thomas yalikuja mnamo 1991 alipotoa wimbo wa kwanza Outstanding, ambao ulifika mpaka namba 12 kwenye UK Singles Chart; wimbo ambao toleo la kwanza ulitolewa na Gap Band.
Mwaka huo huo alifanikiwa kuingiza nyimbo nyingine tatu kwenye chati za UK ikiwemo uliyovuma zaidi Thinking About Your Love ambao ulifika namba 4 kwenye chati hizo na kukaa kwa wiki 13 na wimbo wa Best of You ambao ulifika namba 11 naulidumu kwenye chati kwa wiki saba.
Albamu ya kwanza ya Thomas Voices (1991) ilifikia nambari tatu kwenye chati ya albamu za Uingereza, ikiuza zaidi ya nakala 300,000.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1992 Thomas aliteuliwa kwenye tuzo za kila mwaka za BRIT Awards katika kategoria mbili, mwimbaji bora wa kiume wa Uingereza na mwimbaji chipukizi wa Uingereza.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Gig review: Kenny Thomas at O2 Academy Sheffield". Yorkshire Post (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-04.
- ↑ https://www.crossrhythms.co.uk/articles/music/Kenny_Thomas_Soul_Singer_In_A_Crazy_World/23202/p1/
- ↑ "1990s hitmaker on the road again after Covid battle". Evening News24 (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-15.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kenny Thomas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |