Kampuni ya Magazeti ya Bay State

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kampuni ya Magazeti ya Bay State
Jina la kampuni Kampuni ya Magazeti ya Bay State
Ilianzishwa 1 Mei 1991
Mwanzilishi *. William P. Dole(mmiliki wa hapo awali)
Huduma zinazowasilishwa Uchapishaji
Mmiliki Fidelity Investments
Makao Makuu ya kampuni *. Somerville
*. Massachusetts
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Magazeti ya Kila Wiki
Nchi Marekani Marekani

Kampuni ya Magazeti ya Bay State ina makao yake makuu Somerville, Massachusetts, Marekani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ilikuwa kampuni ya uchapishaji ya magazeti ya kila wiki katika maeneo kaskazini mwa Boston. Iliundwa katika mwaka wa 1991 na kampuni ya Fidelity Investments baada ya kununua kampuni ya Dole Publishing kutoka mmiliki wake wa muda mrefu, William P. Dole.

Kampuni ya Magazeti ya Bay State ilifungwa na kuwekwa katika kitengo cha Metro cha Kampuni ya Magazeti ya Community inayomilikiwa na Fidelity katika mwaka wa 1996. Kampuni ya Magazeti ya Community hivi sasa inamilikiwa na GateHouse Media.

Mali za Bay State zilikusanywa na familia ya Dole, iliyoendesha gazeti la Cambridge Chronicle tangu miaka ya 1930 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1990. Gazeti la Chronicle, gazeti la kuchapisha rekodi za jiji la Cambridge, limechapishwa tangu mwaka wa 1846 na, chini ya usimamizi wa familia ya Dole, likaungana na gazeti shindani la Cambridge Sun.

Familia ya Dole ilinunua pia magazeti makuu ya kila wiki katika miji mingine miwili kaskazini mwa Boston na vilevile kuchapisha majarida mengine mbalimbali.

Mali[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa ununuzi na Fidelity katika mwaka wa 1991, kampuni ya uchapishaji ya Dole (ilibadlishwa jina kuwa Kampuni ya Magazeti ya Bay State) ilihusisha magazeti matatu ya kila wiki, yote yakipatikana katika kata ya Middlesex, Massachusetts.

Magazeti haya yote bado huchapishwa chini ya Kitengo cha Metro cha Kampuni ya Magazeti ya Community. Kampuni ya Bay State ilichapisha jarida dogo la wanunuzi katika eneo la Lowell, chapisho hilo liliitwa Merrimack Valley Advertiser. Chapisho hilo lilibadilishwa baadaye kuwa majarida mawili ya Advertiser katika Tewksbury na Wilmington, haya yanachapishwa, hivi sasa, na Kitengo cha Kaskazini Magharibi chini ya majina ya Tewksbury Advocate na The Wilmington Advocate.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Dole Publishing Is Sold". The Boston Globe, 19 Aprili 1991.
  2. [1]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kampuni ya Magazeti ya Bay State kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.