Kaligrafia
Kaligrafia ni sanaa ya kuandika vizuri na kurembisha maandishi. Neno latokana na lugha ya Kigiriki (καλλιγραφία (kalligrafía) inayounganisha κάλλος (kállos, uzuri, urembo) na γράφειν (gráfein, kuandika)) kupitia Kiingereza calligraphy.
Asili ya kaligrafia iko katika kazi ya kunakili maandiko matakatifu kama vile Korani au Biblia au kutoa hati rasmi. Kabla ya kuanzishwa kwa uchapishaji vitabu vyote viliandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu au burashi.
Katika utamaduni ya Wakristo wa Ulaya waandishi walilenga kutumia herufi nzuri kwa matini kwa jumla waliponakili sehemu za Biblia zilizotumiwa kwa masomo katika makanisa au monasteri. Herufi za kwanza za milango au sehemu maalumu mara nyigi zilipambwa kwa namna ya pekee.[1] Njia nyingine ilikuwa kuongeza picha kando la maneno.
Katika utamaduni wa Uislamu kaligrafia ilipata nafasi ya pekee kwa mapambo ya muswada au majengo kama msikiti na madrasa. [2] Kufuatana na mafundisho ya walimu Waislamu wengi hairuhusiwi kuchora picha ya viumbe na hata kama kuna mifano mingi ya uchoraji picha katika utamaduni wa Kiislamu kwa jumla hautumiwi katika muswada ya kidini na kwenye majengo ya kidini. Badala yake wasanii wa Kiislamu walitumia ayat za Qurani, maneno ya basmala (=bismillah), takbir, majina ya Allah, Muhamad, makhalifa rashidun au maimamu ya Shi'a yanayoandikwa kwa uzuri na kuwa pambo la ukuta au muswada.
Utamaduni wa Asia ya Mashariki hasa China, Korea na Japani inaheshimu sana kaligrafia tangu zamani hadi leo. Maneno au sentensi ya wanafalsafa au ya kidini yanachorwa na kuwekwa kama mapambo katika mabustani nyumbani, kwenye mahekalu au majengo ya umma. Watoto hufundishwa sanaa hii nyumbani na pia shuleni. [3]
-
Kaligrafia katika Vietnam kwa kutumia alama za Kichina zinazochorwa kwa burashi
-
Somo la kaligrafia, Japani karne ya 18
-
Herufi "P" iliyopanushwa na kupambwa katika muswada ya Biblia (chanzo cha neno "Petrus")
-
Kaligrafia ya Kichina katika hekalu ya Sun Yat-sen mjini Taipeh
-
Kichwa pana cha kalamu kwa kaligrafia
References
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.bibliotheca-laureshamensis-digital.de/de/bildergalerie/initialen/zierinitialen.html Mifano ya "initials" (Jer.)
- ↑ Blair, Sheila S.; Bloom, Jonathan M. (1995). The art and architecture of islam : 1250–1800 (Reprinted with corrections. ed.). New Haven: Yale University Press. ISBN 0-300-06465-9.
- ↑ Kuhusu kaligrafia ya China
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Kaligrafos - The Dallas Calligraphy Society, a non-profit guild promoting the calligraphic arts
- Friends of Calligraphy, San Francisco, California
- New Zealand Calligraphers Archived 2 Juni 2018 at the Wayback Machine., a national network of affiliated calligraphy guilds
- The Edward Johnston Foundation Archived 26 Aprili 2023 at the Wayback Machine. - Research centre for calligraphy and lettering arts
- Tovuti kuhusu kaligrafia ya Kiislamu Archived 8 Juni 2012 at the Wayback Machine.