Basmala
Mandhari
Basmala (Ar. بسملة basmala) ni jina kwa maneno ya Bismillah (بسم الله "Kwa jina la Mungu/Allah", kamili "b-ismi-llāhi r-raḥmāni r-raḥīmi") ambayo ni maneno ya ufunguzi kwa sura za Qurani[1]. Ar-rahman („mwenye rehema“) na Ar-rahim („mwenye neema“) ni pia kati ya majina 99 ya Allah.
Waislamu hutumia maneno haya mara nyingi kwa mfano kila wanapoanza sala au kazi muhimu kama vile kabla ya kula chakula, kabla ya safari, wakati wa kuingia katika msikiti, wakati wa kuzika maiti.
Katika sanaa ya Kiislamu basmala hutumiwa mara nyingi kama kaligrafia.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Basmala kama kaligrafia ya Kiarabu
-
Basmala kama kaligrafia kwa umbo la tunda
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kila sura ya Qurani isipokuwa sura ya 9 inaanza kwa maneno "b-ismi-llāhi r-raḥmāni r-raḥīmi" yaani "kwa jina la Mungu mwingi wa ehema mwenye kurehemu"
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Bismillah Samples, a collection of bismillah art-forms.
- Bismallah Ilihifadhiwa 19 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. in Tadabbur-i-Qur'an.
- Meaning of Bismillah
- Beyond Probability, God's Message in Mathematics. Series 1: The Opening Statement of the Quran (The Basmalah).