Nenda kwa yaliyomo

Jumanne Mhero Ngoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jumanne Mhero Ngoma[1] (Makanya, Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania[2], 1939 - Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam [3], 30 Januari 2019) ni mtu ambaye serikali ya Tanzania inasema aligundua madini ya Tanzanite. Ngoma alifariki akiwa na umri wa miaka themanini[2].

Ugunduzi wa Tanzanite

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka 1967, alipokuwa na miaka ishirini na nane[2], Ngoma alikwenda Kiteto kutembelea familia yake. Aligundua madini ya buluu alipotembea nje. Akaleta madini hayo katika basi mpaka Nairobi, Kenya – jiji ambalo lilitafiti madini zaidi ya Arusha - lakini watu wa Nairobi hawakuweza kugundua madini yake yalikuwa ya aina gani[4]. Baadaye, madini hayo yalipelekwa Dodoma ili kuchunguzwa katika maabara. Huko, Ian MacCloud (mwanajiolojia) alisema madini yale yalikuwa aina ya Zoisite[5]. Katika mwaka 1968, mwaka mmoja baada ya ugunduzi wa madini ya Tanzanite, duka la vito linaloitwa Tiffany & Co. lilianza kuuza madini hayo na kuyapa jina la “Tanzanite”[6].

Tanzanite: Madini ambayo yaligunduliwa na Jumanne Mhero Ngoma.

Tuzo kwa ugunduzi

[hariri | hariri chanzo]

Miaka kumi na tatu baada ya ugunduzi wake, katika 1980, Mzee Ngoma alipewa cheti na shilingi elfu hamsini kutoka rais wa nchi ya Tanzania kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere[3]. Shilingi elfu hamsini ni sawa na kama dola ishirini na mbili leo[1]. Mzee Ngoma aliheshimiwa na rais Jakaya Kikwete pia katika mwaka 2015[5]. Miaka hamsini na moja baada ya kugundua Tanzanite, Mzee Ngoma alipata zawadi kubwa kwa ugunduzi wake. Tarehe 6 Aprili 2018, rais wa nchi ya Tanzania John Magufuli alimpa Mzee Ngoma shilingi milioni mia moja[3].

Tafsiri tofauti kuhusu ugunduzi

[hariri | hariri chanzo]

Jumanne Mgoma ni mtu ambaye serikali ya Tanzania inasema aliona madini cha Tanzanite kwanza. Lakini, watu wengine wanasema kwamba mtu wa kabila la Wamasai, Ali Juuyawatu, aligundua Tanzanite na alimuambia Manuel D’Souza, mtaalamu wa madini[7].

Zaidi kuhusu Tanzanite

[hariri | hariri chanzo]

Madini ya Tanzanite yana thamani kubwa kwa sababu inapatikana katika nchi ya Tanzania tu – hakuna Tanzanite katika nchi yoyote nyingine[2] - tena ndani ya eneo la kilomita za mraba nane tu katika mkoa wa Manyara karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Pia, watu baadhi wanafikiri kwamba hakutakuwa na madini ya Tanzanite zaidi baada ya miaka kumi na tano kutoka sasa. Kwa hivyo, madini ya Tanzanite ni adimu sana[7].

  1. 1 2 "Tanzanian gemstone finder living in poverty". www.aa.com.tr. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  2. 1 2 3 4 Mweha Msemo (2019-02-03). "Face2Face Africa News - Face2Face Africa News %". Face2Face Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  3. 1 2 3 "Tanzanite discoverer, Ngoma, dies at Muhimbili". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  4. "Govt moves to recognise Mzee Ngoma's discovery of tanzanite". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  5. 1 2 "Tanzanite discovery hits 51th anniversary". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  6. The Tanzanite Experience. (2019, October). Discovery of Tanzanite. https://www.tanzaniteexperience.com/2019/10/
  7. 1 2 "A Rare and Beautiful Stone Fails to Shine: Tanzania's Missed Opportunity". Knowledge at Wharton (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.