Juliani wa Ainvarza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Juliani.

Juliani wa Ainvarza (Istria, 231 - Ainvarza, Kilikia, leo nchini Uturuki, 22 Juni 249) alikuwa mvulana ambaye aliteswa muda mrefu kwa ajili ya imani yake ya Kikristo wakati wa dhuluma ya Decius, kaisari wa Dola la Roma; hatimaye alitoswa baharini ndani ya gunia lililojaa nyoka[1].

Vyanzo vingine vinasema alitokea Tarso na kuuawa chini ya kaisari Dioklesyano.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kati ya watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Machi[2] au 18 Aprili au 21 Juni.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.