Nenda kwa yaliyomo

Joshua King

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joshua King.

Joshua Christian King (alizaliwa 15 Januari 1992) ni mchezaji wa soka wa Norway ambaye anacheza kama mshambuliaji wa Klabu ya Ligi kuu ya Uingereza iitwayo AFC Bournemouth na timu ya taifa ya Norway.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

King alisainiwa na Klabu ya Manchester United kutoka katika Klabu ya Vålerenga mnamo mwaka 2008. Baada ya kwenda kwa mkopo katika Klabu ya Preston North End na baadaya kutumikia Klabu mbalimbali kama vile Borussia Mönchengladbach, Hull City na Blackburn Rovers zote hizi alizitumikia kwa mkopo,na baadaye alisaini kabisa katika Klabu ya Blackburn mnamo Januari 2013, kabla ya kuhamia Bournemouth mnamo Mei 2015.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alianza kuiwakilisha timu ya taifa ya Norway akiwa na umri wa chini ya miaka 16, na baadaye aliiwakilisha chini ya miaka 18 na hatimaye aliiwakilisha tena chini ya miaka 21, King alicheza kwa mara yake ya kwanza katika mechi ya kimataifa dhidi ya Iceland mnamo 2012, na aliweza kufunga goli lake la kwanza la kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Cyprus.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joshua King kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.