Josefa Francisco
Josefa "Gigi" Francisco (1954 - 22 Julai 2015) [1] alikuwa mtetezi wa usawa wa kijinsia, haki ya kijamii, na haki za wanawake kutoka Ufilipino . [2] Alichangia programu nyingi za kupunguza unyanyasaji wa usawa na kufanya utafiti juu ya vipengele vingi vya usawa kwa wanawake. Gigi alifanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa katika miradi mbalimbali.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Kupitia ufundishaji na uandishi wake, alianzisha uzoefu wa kiufundi, maono na harakati za kijamii kwa kizazi kipya. Aliwahi kuwa mwanachama wa ISIS International kuanzia mwaka 1998 hadi 2002. Shirika linafanya kazi juu ya haki za wanawake Kimataifa. Baadaye, alijiunga na taasisi ya Wanawake na Jinsia (WAGI) kama mkurugenzi mtendaji wa shirika. Shirika hilo limekuwa likifanya kozi mbalimbali za mtandaoni kuhusu haki za wanawake. Alikuwa mwanachama wa Shirika la Mibadala ya maendeleo kwa Wanawake katika Enzi Mpya, iliyofupishwa kama DAWN. Shirika hilo linafanya kazi ya kueneza sauti na mitazamo ya wanawake kutoka kanda ya kusini duniani kote. Alihudumu kama mratibu wa kimataifa wa shirika. Umoja wa Mataifa na DAWN zilifanya kazi pamoja katika eneo la Asia-Pasifiki chini ya uongozi wa Gigi.
Alifanya kazi kama mkuu wa idara ya Mafunzo ya Kimataifa katika Chuo cha Miriam, akifanya kazi ya kukuza uongozi wa wanawake. [3] Alifanya utafiti muhimu kuhusu umaskini, jinsia, maendeleo na harakati za utetezi wa haki za wanawake. [4]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Josefa "Gigi" Francisco". AWID (kwa Kiingereza). 2015-11-25. Iliwekwa mnamo 2020-03-12.
- ↑ "Josefa "Gigi" Francisco, In Remembrance". 24 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Josefa "Gigi" Francisco, In Remembrance". 24 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 10 Machi 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Josefa "Gigi" Francisco, In Remembrance". 24 July 2015 - ↑ Joanna Kerr, Ellen Sprenger, Alison Symington (2004). The Future of Women's Rights: Global Visions and Strategies. Zed Books. uk. 69. ISBN 1842774581.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Josefa Francisco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |