Nenda kwa yaliyomo

Joho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joho la jioni la huko Paris, Ufaransa, 1823.
Maaskofu Walutheri wa Udani wenye kuvaa joho juu ya mavazi mengine.

Joho (kwa Kiingereza: "cloack") ni vazi pana linalofanana na koti refu ambalo mbele liko wazi. Aghalabu hushonwa au hunakshiwa kwa darizi katika sehemu za shingoni na mbele.

Joho hunakshiwa kwa rangi mbalimbali, kwa mfano nyeusi au bluu.

Barani Afrika joho huvaliwa hasa kwenye mahafali baada ya kumaliza elimu ya juu.

Katika madhehebu kadhaa ya Ukristo linatumika katika ibada mbalimbali, pengine kwa jina la "pluviale" (yaani "nguo ya mvua"; kwa Kiingereza: "cope").

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joho kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.