John George Kemeny
Mandhari
John George Kemeny (31 Mei 1926 - 26 Desemba 1992) alikuwa mtaalamu wa kompyuta anayekumbukwa kwa kuunda lugha ya BASIC pamoja na Thomas Eugene Kurtz kwenye Chuo cha Dartmouth, mnamo mwaka 1964.
Alizaliwa Budapest, Hungaria katika familia ya Kiyahudi na mwaka 1940 familia yake ilikimbilia Marekani wakati Hungaria (iliyoshiriki na Ujerumani wa Adolf Hitler) iliandaa sheria dhidi ya Wayahudi.
Tangu mwaka 1945 alisoma hisabati na falsafa kwenye Chuo Kikuu cha Princeton; wakati wa kutunga tasnifu ya uzamivu alifanya kazi kama msaidizi wa Albert Einstein.
Aliendelea kufundisha kwenye Chuo cha Dartmouth. Kuanzia mwaka 1963 aliunda hapa lugha ya kompyuta BASIC kwa shabaha ya kuwezesha watu wengi kutumia kompyuta.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John George Kemeny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |