Jill Roord
Mandhari
Jill Jamie Roord RON (alizaliwa Aprili 22, 1997) ni mchezaji wa mpira wa miguu ambae anacheza kama kiungo katika klabu ya wanawake ya VfL Wolfsburg katika ligi ya Frauen-Bundesliga nchini Ujerumani na timu ya taifa ya wanawake ya nchini Uholanzi. Awali alicheza katika timu ya wanawake ya Arsenal nchini Uingereza, Bayern Munich katika Ligi ya Ujerumani na alishinda mataji mengi ya kitaifa na timu ya FC Twente ya nchini Uholanzi. Wakati wa msimu wa 2015-16 kwenye ligi ya Eredivisie, alikuwa mchezaji bora katika ligi hiyo.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Hoe het WK-doelpunt van Jill Roord het leven van haar familie (even) op zijn kop zette", AD, June 13, 2019.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jill Roord kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |