Nenda kwa yaliyomo

Jennifer Mgendi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jennifer Mgendi
Amezaliwa 2 Mei 1972
Dar es Salaam
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwimbaji


Jennifer Mgendi (alizaliwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, Tanzania, 2 Mei 1972) ni mwimbaji wa nyimbo za Injili na pia ni mwigizaji[1].

Baba yake anaitwa Fanuel Mgendi na mama yake anaitwa Mwendapelu Nalaila. Pia ana ndugu zake wa damu watatu ambao ni Mao, Mlenge na Noel.

Amefunga ndoa na Dr. Job Chaula mwaka 1998 na wamebarikiwa kupata watoto watatu ambao ni Jotham, Jefta na Joan.

Elimu yake

[hariri | hariri chanzo]

Alianza elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mgulani, baada hapo aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya wasichana ya Kisutu. Pia amepata elimu yake ya juu katika chuo cha ualimu cha Korogwe na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kazi zake

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya kazi alizowahi kufanya katika tasnia ya uigizaji na uimbaji ni pamoja na:

  • Nini - 1995
  • Ukarimu wake - 2000
  • Nikiona fahari - 2001
  • Yesu nakupenda - 2004
  • Mchimba mashimo - 2006
  • Kiu ya nafsi - 2009
  • Hongera yesu - 2013
  • Pigo la faraja
  • Teke la mama
  • Chai moto
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jennifer Mgendi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.