Jenista Joakim Mhagama
Jenista Joakim Mhagama (amezaliwa 23 Juni 1967) ni mbunge wa jimbo la Peramiho katika bunge la kitaifa nchini Tanzania.[1] Anatokea katika chama cha CCM.
Pia amekuwa Waziri katika serikali ya awamu ya tano[2] na ya sita vilevile.
Desemba 2015, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu katika utawala wa Rais John Magufuli. Mnamo Januari 2022, alihamishwa hadi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Huduma za Umma.[3]
Elimu na kazi
[hariri | hariri chanzo]Jenista Mhagama alimaliza elimu yake katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Peramiho mwaka 1986. Mwaka 1989, alipata Diploma ya Elimu kutoka Chuo cha Ualimu Korogwe.
Alifanya kazi kama mwalimu kwa miaka sita kati ya 1991 na 1997.[4]
Maisha ya siasa
[hariri | hariri chanzo]Mhagama alianza kujihusisha na CCM mwaka 1987 na kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo za tawi la vijana na wanawake wa chama hicho. Aliteuliwa kwa mara ya kwanza katika Bunge kuwa mbunge wa viti maalum kilichotengwa kwa ajili ya wanawake mwaka wa 2000.[5]
Mwaka wa 2005, alimshinda aliyekuwa Waziri wa Fedha Simon Mbilinyi katika mchujo wa haki ya kuiwakilisha CCM katika uchaguzi ujao wa jimbo la Peramiho. Ilitokana na uchambuzi uliogundua kuwa Mhagama alikuwa mbunge wa pili kwa wingi wa michango ya mijadala na maswali kwa mawaziri katika Bunge la 2005-2010.[6]
Mhagama alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete kati ya Januari 2014 na Januari 2015. Kisha katika mabadiliko ya baraza la mawaziri alipandishwa cheo na kutajwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, uratibu na Bunge).[7]
Katika uchaguzi mkuu wa 2015, Mhagama alishinda kiti chake cha Peramiho dhidi ya mgombea wa CHADEMA Erasmo Mwingira kwa kura 32,057 dhidi ya 11,462.[8]
Katika baraza jipya la mawaziri la Rais John Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu wa Kimwili).
Mnamo Januari 2022, alihamishwa hadi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Huduma za Umma.[9]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mengi kuhusu Jenista Joakim Mhagama". 21 Julai 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-20. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/nani-ni-nani-serikali-ya-jpm-jenista-mhagama/1596774-3039628-1234fil/index.html Gazeti la Mwananchi (Januari 19, 2016) Jenista Mhagama – Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-09. Iliwekwa mnamo 2024-05-08.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ https://web.archive.org/web/20150722024644/http://www.parliament.go.tz/index.php/members/mpcvs/1155/2010-2015
- ↑ https://web.archive.org/web/20150722024644/http://www.parliament.go.tz/index.php/members/mpcvs/1155/2010-2015
- ↑ https://archive.today/20130418223110/http://www.dailynews.co.tz/home/?n=13930&cat=home
- ↑ https://web.archive.org/web/20161021074148/http://www.thecitizen.co.tz/News/national/Two-new-faces-in-Kikwete-s-cabinet/1840392-2601552-3ein4v/index.html
- ↑ https://web.archive.org/web/20151126095523/http://www.nec.go.tz/uploads/documents/1448025692-MALIMA-WABUNGE.pdf
- ↑ https://web.archive.org/web/20161021071408/http://www.dailynews.co.tz/index.php/home-news/45019-new-ministers-for-swearing-in-on-saturday
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |