Jean-Claude Iranzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jean-Claude Iranzi

Jean-Claude Iranzi (alizaliwa 5 Oktoba 1990) ni mchezaji wa soka, ambaye kwa sasa anachezea katika klabu ya ZESCO United FC kwenye Ligi Kuu ya Zambia na timu ya taifa ya Rwanda kama mshambuliaji .

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

SC Kiyovu Sport[hariri | hariri chanzo]

Mshambuliaji huyo alianza kazi yake mnamo 2004 alijiunga na klabu ya SC Kiyovu Sport na alipandishwa kwenye timu ya Ligi ya kombe la Shirikisho nchini Rwanda mwaka 2006. Alicheza kwa mara yeke ya kwanza katika klabu hiyo ya SC Kiyovu Sport mnamo Juni 2006.

APR FC[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Desemba 2008, Iranzi alisaini mkataba na klabu ya APR FC, wakiwa kama mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda. Alicheza klabu hiyo ya APR FC katika mechi iliyopangwa ya kirafiki dhidi ya Polisi FC.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Iranzi alicheza Mashindano ya Vijana ya chini ya miaka 20 mnamo 21 Juni 2008 kwenye mechi ya kufuzu katika Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2010 dhidi ya timu ya taifa ya Moroko.

Iranzi alifunga goli la kwanza la kimataifa mnamo 26 Machi 2011 kaatika mechi ya kufuzu katika Kombe la Mataifa ya Afrika ,Goli hilo lililofungwa dakika ya 44, liliipa Rwanda ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa kikanda Burundi.


Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jean-Claude Iranzi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.