Jean-Bedel Bokassa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jean Bedel Bokassa (22 Februari 1921 - 3 Novemba 1996) alikuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na baadaye Kaisari WA Milki ya Afrika ya Kati hadi alipopinduliwa tarehe 21 Septemba 1979.

Mwanajeshi[hariri | hariri chanzo]

Bokassa alizaliwa Bobangi akajiunga na jeshi la kikoloni la Ufaransa. Hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alipanda ngazi akafikia cheo cha afande. Hadi 1961 akawa kepteni. 1964 alitoka katika jeshi la Ufaransa akaingia katika jeshi la jamhuri changa ya Afrika ya Kati. Akiwa ndugu wa rais David Dacko akaendelea kupanda ngazi hadi kuwa mkuu wa jeshi.

Rais na dikteta[hariri | hariri chanzo]

Tar. 1 Januari 1966 Bokassa akampindua rais Dacko akajitangaza kuwa rais mpya akafuta katiba ya nchi. Bokassa alisaidiwa mara kadhaa na Ufaransa. Mwaka 1967 aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Wafaransa ili apate kuimarisha utawala wake.

1972 Bokassa akajitangaza kuwa rais wa maisha. Aliona majaribio mbalimbali ya kumpindua au kumwua lakini kwa jumla ni wapinzani wake waliopaswa kuaga dunia.

Katika miaka ya 1970 Bokassa alitafuta usaidizi wa Libya akasilimu baada ya kumtembelea Rais Gadhaffi akajiita Salah Eddine Ahmed Bokassa.

Kaisari[hariri | hariri chanzo]

Septemba 1976 Bokassa aliachicha serikali yake akaanzisha "Halmashauri ya Mapinduzi ya Afrika ya Kati": 4 Desemba 1976 akatangaza jamhuri kuwa milki na weyewe kuwa Kaisari kwa mfano wa Napoleoni. Bokassa alirudi katika kanisa katoliki, akawaalika wageni wengi na katika sherehe iliyogharamia dollar milioni 30 akajiwekea taji la Kaisari "Bokassa I".

Serikali yake iliendelea kuwa ya kidikteta. Wapinzani waliuawa hovyo au kupotea magerezani.

Ufaransa iliendelea kumsaidia.

Mapinduzi[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Januara na Aprili 1979 wanafunzi waliandamana. Upinzani huu ulikandamizwa kwa msaada wa jeshi la Kongo. Wanafunzi wengi walikamatwa wengine kupigwa sana na kuuawa. Kwa jumla ni wanafunzi na watoto zaidi ya 100 waliuawa.

Katika hali hii Bokassa alisafiri tena kwenda Libya. Wapinzani walichukua nafasi ya kumpindua Bokassa wakiongozwa na aliyewahi kuwa raisi David Dacko tar. 21 Septemba 1979. Milki ilifutwa na Jmahuri kurudishwa.

Mwisho gerezani[hariri | hariri chanzo]

Bokassa alipewa hukumu ya mauti lakini hakuhudhuria kesi. Aliporudi mwaka 1986 alikamatwa na kuhukumiwa tena afe. Adhabu ilipunguzwa baadaye kuuwa miaka 20.

Mwacha 1993 aliachishwa gerezani na rais André Kolingba akaishi miaka kadhaa akafa 3 Novemba 1996 huko Bangui. Bokassa aliacha wake 17 na watoto 50.