Jaribio la kumuua Donald Trump
Jaribio la kumuua Donald Trump, rais wa 45 wa Marekani na mteule wa Chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, lilifanyika tarehe 13 Julai 2024, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi, karibu na mji wa Butler, Pennsylvania. [1] Hata hivyo Donald Trump amenusurika kifo katika jaribio hilo ambapo amepigwa risasi upande wa juu wa sikio lake la kulia.
Aliyefanya jaribio hilo la kumuua alitambuliwa kwa jina la Thomas Matthew Crooks mwenye umri wa miaka 20, mkazi wa Bethel Park, Pennsylvania. [2] [3] [4] Maafisa usalama na mashuhuda walisema kwamba jahili alifyatua risasi kutoka kwenye paa la jengo la jirani ya uwanja wa mkutano kwa kutumia bunduki ya nusu-otomatiki aina ya AR-15, na kufyatua risasi nane kabla ya kuuawa na mdunguaji kutoka Kikosi cha Kijasusi cha Serikali . [5] [6]
Baada ya kupigwa risasi, Trump alichumpa chini na alizingirwa haraka na Maofisa Walinzi ; aliinuka huku akivuja damu nyingi kwenye sikio lake la kulia, akafanya ishara ya kusukuma ngumi hewani mara kadhaa kabla ya kukimbizwa kwenye gari. [7] Kisha alipelekwa hospitali na kuruhusiwa akiwa katika hali nzuri, na baadae akaondoka kwa ndege kwenda New Jersey . [8] [9] Mshiriki mmoja wa mkutano aliuawa, na wengine wawili walijeruhiwa vibaya.
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Rais wa zamani Donald Trump ndiye mteule wa kugombea urais kupitia chama cha Republican katika Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 2024 . [10]
Mnamo Julai 5, 2024, ilitangazwa kuwa Trump atapokea maandamano katika Viwanja vya Maonyesho ya Shamba la Butler kati ya mji wa Connoquenessing na Meridian karibu na Butler, Pennsylvania, tarehe 13. [11] [12] Ilifanyika kama sehemu ya kampeni ya urais ya Trump kwa ajili ya uchaguzi ili kuongeza kura katika jimbo la Pennsylvania ; jimbo ambalo lina kura 19 za Makada wa Chama, na kura 270 zinahitajika ili kuchaguliwa kuwa Rais. [13] Mwenyekiti wa Kamati ya Republican ya Kaunti ya Butler James E. Hulings alikadiria watu 50,000 walikuwa kwenye mkutano huo. Mwakilishi Mike Kelly alisema kuwa alijaribu kuwasiliana na kampeni ya Trump kuwa wabadilishe eneo la mkutano huo liwe kwenye eneo ambalo linaweza kumudu umati mkubwa kuliko Uwanja wa Butler Farm Show. Alidai walimjibu kwa kumwambia, "Tunashukuru kwa mchango wako lakini tayari tumesha amua." Shambulio likatokea siku mbili kabla ya kuanza kwa Kongamano la Kitaifa la Republican la 2024 . [13] Mikutano ya Trump huwa inakaguliwa ili kudhibiti vitu vilivyopigwa marufuku, kama silaha. [14]
Trump alipigwa risasi ikiwa ni takriban saa 12:11 jioni EDT [17] [18] wakati wa mkutano wake wa kampeni. [19] Dakika sita baada ya Trump kuanza kuhutubia, Thomas Matthew Crooks alifyatua risasi nane kwa kutumia bunduki aina ya AR-15 kwenye mkutano huo. [17] [18]Jahili hakufanyiwa uchunguzi wa usalama kwa vile alikuwa nje ya eneo la usalama wa mkutano huo; alikuwa amepanda juu ya paa la jengo, feet 200 hadi 400 (m 61 hadi 122) kaskazini mwa Trump. [20] [21] Mfanya shambulio aliuawa na mdunguaji wa Kikosi cha Kupambana na Mashambulio ya Siri cha Marekani mara baada ya kupigwa risasi.
Shambulio
[hariri | hariri chanzo]Siku ambayo jaribio hilo lilifanyika, Thomas Matthew Crooks alimuazima baba yake bunduki aina ya rifle—ya kundi la DPMS Panther Arms - toleo la AR-15– yenye mtutu wa nchi 16 na chemba ya kipimo cha 5.56×45mm NATO, ambayo ingeweza kufanya kazi hiyo kama alivyotaka Crooks. Maofisa wa Serikali Kuu ya Marekani wameieleza silaha hiyo kuwa ni ya kiwango cha kawaida.[22][23][24] Baadae akanunua risasi 50 kutoka kwenye duka la silaha[22] na akanunua ngazi ya futi 5 (meta 1.5) kisha akaendesha gari yake kuelekea eneo la mkutano huku akiwa amepakia zana za milipuko.[25] Akapanda juu ya paa la jengo jirani, urefu wa takriban futi 400 (meta 120) kaskazini ya lilipokuwepo jukwaa. Jengo hilo lilikuwa chini ya uangalizi wa maofisa polisi 3, lakini hakukuwa na aliyepangwa kulinda kwa juu kutokana na upungufu wa rasilimali watu wa kiulinzi. Crooks hakupitia ukaguzi wa wanausalama kwa kuwa, kwa mujibu wa maofisa wenyewe, jengo hilo lilikuwa nje ya wigo wao wa uangalizi wa maandamano .[26]Kwa mujibu wa WPXI, Crooks alipigwa picha mara mbili na maofisa usalama kabla ya tukio la ufyatuaji risasi. Kabla ya saa 11.45 jioni, saa za eneo hilo, ofisa wa polisi alimuona Crooks kabla hajapanda juu na alitoa ripoti aliyoambatisha na picha, kuwa ni mtu wa kutilia shaka. Ofisa mwingine akamtafuta Crooks lakini hakumuona. Vyanzo kadhaa vya vyombo vya kiulinzi vya eneo hilo navyo vimeripoti kuwa vilitilia shaka uwepo wa Crooks kwenye eneo lililokuwa na vifaa vya kiteknolojia viitwavyo magnetometers; wakatumia simu ya upepo kuripoti, na kumbukumbu za mawasiliano hayo zimewasilishwa kwa Shirika la Kijasusi.
Saa 11.45 jioni, mmoja wa wanatimu ya Masuala ya Kiufundi Kitengo cha Matukio ya Dharura cha Beaver County, Pennsylvania, alimuona Crooks juu ya paa, akawajulisha maofisa wenzake, na kumpiga picha. Katika moja ya matukio mawili ambayo Crooks alipigwa picha, afisa polisi aliyempiga picha alimuona akiliangalia eneo kama afanyaye mpango fulani akiwa juu ya paa ameshika kifaa cha kuvutia taswira karibu.[27][28] Makachero wa usalama walimuona Crooks juu ya paa takriban dakika 20 kabla ya tukio la ufyatuaji risasi.[29] Repoti zinaonesha kulikuwa na mashuhuda kadhaa waliomuona na bunduki akiwa juu ya paa wakawafahamisha polisi takriban dakika moja na nusu kabla ya ufyatuaji risasi dhidi ya Trump.[30][31] Afisa mmoja wa polisi wa mji wa Butler alijaribu kumpandia Crooks juu ya paa alikokuwa, akisaidiwa na afisa mwingine. Crooks akamuona afisa huyo akati mikono ya afisa ikiwa ingali inashikilia kingo za paa, akamlenga na bunduki, na afisa ikambidi ajiachie na kuanguka (meta 2.4) na kujiumiza vibaya kiwiko cha mguu. Crooks akaanzisha shambulio la kutaka kuua punde tu baada ya kukabiliana na afisa huyo.[32][33][34]
Iran yakanusha shutuma za kula njama
[hariri | hariri chanzo]Siku ya Jumatano ya Julai 17 2024, taifa la Iran limekanusha vikali lilichokiita 'uchokozi' wa dhahiri uliofanywa na vyombo vya habari vya Marekani kwa kulihusisha taifa hilo na njama za kumuua Donald Trump.[35]
Siku ya Jumanne (16 Julai) CNN iliripoti kuwa maafisa wa serikali ya Marekani walipokea taarifa za kiintelijensia kutoka kwa mtu mmoja, wiki chache nyuma, kuwa Iran inaweza kuwa inafanya njama dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, jambo lililochagiza uimarishaji wa ulinzi wa Trump. Mashirika mengine ya utangazaji ya Marekani pia yalitangaza shutuma hizo.[35]
Hata hivyo CNN ilifafanua baadae kuwa shutuma dhidi ya Iran hazihusiani hasa na tukio la kujaribu kumuua Trump. Hali kadhalika Kamati ya Kitaifa ya Ulinzi ya Marekani imesema kuwa kwa miaka mingi, imekuwa ikiifuatilia kwa karibu Iran hasa kutokana na vitisho vya nchi hiyo vya kuulipizia kisasi uliokuwa utawala wa Trump, baada ya utawala huo kufanya shambulizi lililomuua Jenerali wake mwanamapinduzi, Qassam, mwaka 2020.
Taarifa zaidi
[hariri | hariri chanzo]Jahili alikuwa hatua moja mbele
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 28 Julai, The New York Times liliripoti kuwa mfanya shambulio la bunduki kwenye mkutano wa Trump aliwazidi makachero kimbinu. Kupitia arafa ambazo gazeti hilo ilizipata katika namna ya kipekee, zilionesha kuwa maofisa usalama walikuwa na tetesi juu ya Thomas Crooks mapema zaidi kuliko ilivyokuwa ikifahamika. Naye [Crooks] alilijua hilo.[36]
Pia kuna jambo lipo tofauti: zilipita dakika 90 tangu alipogundulika hadi pale alipouwawa, na si dakika 60 kama maafisa usalama walivyokuwa wakisema kupitia vyombo vya habari. Alionekana kwa mara ya kwanza saa 10.26 jioni. Alipigwa picha kwa mara ya kwanza saa 11.14 jioni na aliuwawa saa 12.11 jioni.
Taarifa zimebainisha kuwa mara nyingi jahili huyo "amekuwa hatua moja mbele" ya maofisa usalama. Bw. Crooks alilipeleleza eneo la mkutano siku moja kabla ya maofisa usalama nao kufanya hivyo. Alitumia droni kufanya upelelezi kwenye eneo hilo wakati maofisa usalama hawakujaribu hata kutafuta idhini ya kufanya hivyo. Crooks alifanya utafiti juu ya umbali aliokuweko Lee Harvey Oswald kutoka alikokuwa John F. Kennedy alipomfanyia mauaji rais huyo wa zamani mwaka 1963 - akapata jibu kuwa ni takriban futi 265 - na alifanikiwa kukwea futi 400 juu ya jengo na kupata ukaribu zaidi na Trump; paa ambalo wana usalama waliliacha bila ulinzi.[36]
Kwa hiyo, wakati wanausalama wanayaangalia maandamano, Crooks alikuwa akiwaangalia wao; na baada ya tukio polisi walipagawa na kujiuliza: alifanyaje fanyaje?!
Kuenea kwa uvumi wa kula njama
[hariri | hariri chanzo]Wachambuzi wa masuala ya ulaji njama walijitokeza mapema sana mara baada ya tukio la Trump kunusurika kifo. Wana-nadharia hao wa matukio ya ulaji njama walidai kuwa jaribio hilo la kumuua Donald Trump lilipangwa na ilitumika damu feki.[37]
Ikiwa zimepita dakika chache tu tangu tukio litokee, wana-nadharia hao waliweka machapisho kwenye mitandao ya kijamii hasa ule wa X wakidai kuwa jaribio hilo lilipangwa ili kuchechemua mkakati wa Trump kushinda uchaguzi.[37]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Trump shot in right ear at campaign rally, shooter dead".
- ↑ Barnes, Julian E.. "Live Updates: Trump 'Safe' After Shooting at Rally; Suspect Killed", July 13, 2024. (en-US)
- ↑ "FBI identifies Thomas Matthew Crooks as 'subject involved' in Trump rally shooting", 14 July 2024.
- ↑ Gurman, Sadie. "Law Enforcement Identifies Thomas Matthew Crooks, 20, as the Suspected Shooter", 14 July 2024.
- ↑ "Videos Show Suspect Lying Motionless on Nearby Rooftop After Shooting", July 13, 2024.
- ↑ Tanyos, Faris (Julai 13, 2024). "Trump rally shooter killed by Secret Service sniper, officials say - CBS News" (kwa American English). CBS News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Layne, Nathan (Julai 13, 2024). "Trump shot in right ear at campaign rally, shooter dead". Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hayes, Christal. "Trump, with blood on face, raises fist in air". BBC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Live updates: Trump says he was shot in the ear during rally; one attendee and shooter are dead". AP News (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 13, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kinnard, Meg. "Biden and Trump are now their parties' presumptive nominees. What does that mean?", March 13, 2024.
- ↑ Trizzino, Eddie (2024-07-05). "Trump to campaign at Butler Farm Show". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo 2024-07-14.
The rally is scheduled to begin at 5 p.m. at the Butler Farm Show grounds, 625 Evans City Road in Connoquenessing Township.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Donald Trump to hold rally in Butler, Pa. ahead of 2024 election". 90.5 WESA (kwa Kiingereza). Julai 12, 2024. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 13.0 13.1 "Trump returning to Western Pennsylvania just two days before GOP convention". Pittsburgh Post-Gazette (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Gold, Michael (Julai 13, 2024). "Trump 'Safe' After What Sounded Like Gunshots at Rally". The New York Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 13, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Shooting at a Trump Rally in Pennsylvania: Maps and Photos", The New York Times, July 13, 2024. (en-US)
- ↑ "Trump injured, rushed from stage after shooter fired on his Pennsylvania rally", July 13, 2024. (en)
- ↑ 17.0 17.1 Katersky, Aaron. "Trump rally shooter used AR-15-style rifle, Secret Service says". ABC News (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 18.0 18.1 Powell, Tori B. (Julai 13, 2024). "Live updates: Trump injured in shooting at Pennsylvania rally that left at least 1 dead | CNN Politics" (kwa Kiingereza). CNN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 13, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Perez, Jeremy Herb, Jeff Zeleny, Holmes Lybrand, Evan (Julai 13, 2024). "Trump injured in shooting at Pennsylvania rally | CNN Politics" (kwa Kiingereza). CNN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Watson, Kathryn (Julai 13, 2024). "Trump says bullet 'pierced the upper part of my right ear' when shots were fired at Pennsylvania rally - CBS News" (kwa American English). CBS News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Possible security lapses in focus after Trump rally shooting". Julai 13, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 13, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 22.0 22.1 Thomas, Pierre; Katersky, Aaron; Shalvey, Kevin; Barr, Luke (Julai 17, 2024). "New details emerge in Trump assassination attempt investigation". ABC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 16, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Penzenstadler, Nick (Julai 16, 2024). "AR rifle used in Trump shooting from company with winding history, campaign visit". USA Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 16, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McCardle, Guy D. (Julai 16, 2024). "SOFREP Reports: The Weapon Used in the Trump Assassination Attempt Revealed". sofrep.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 16, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "A shooting range, a gun store, and a ladder purchase: Tracking the Trump rally gunman's movements leading up to his attack", CNN, July 15, 2024.
- ↑ Ray, Siladitya (Julai 16, 2024). "Three Snipers Were Inside Building Trump Rally Shooter Fired From, Reports Say". Forbes. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 16, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Paul, John (Julai 15, 2024). "Exclusive: County Officer Warned of Seeing Man With Rangefinder Before Trump was Shot". Beaver County News. Iliwekwa mnamo Julai 18, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Secret Service was told police could not watch building used by Trump rally shooter".
- ↑ "Secret Service spotted Trump rally shooter on roof 20 minutes before gunfire erupted", ABC News.
- ↑ O'Donoghue, Gary (Julai 14, 2024). "Trump rally: Witness says he saw gunman minutes before shots were fired". BBC News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Witnesses warned police of Trump shooter at least 86 seconds before gunfire, video shows", July 15, 2024.
- ↑ Carr Smyth, Julie; Colvin, Jill; Long, Colleen; Balsamo, Michael; Tucker, Eric; Price, Michelle L. (Julai 14, 2024). "FBI investigating Trump rally attack as potential act of domestic terrorism". Associated Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 15, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Borrasso, Jennifer (Julai 14, 2024). "Butler Township officer encountered Trump rally shooter on roof, Butler County sheriff says". CBS News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 15, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 15, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Scolforo, Mark; Tucker, Eric; Kunzelman, Michael (Julai 15, 2024). "Signs of trouble at Trump rally were evident in minutes before gunman opened fire". Associated Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 15, 2024. Iliwekwa mnamo Julai 15, 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 35.0 35.1 "Iran rejects accusations implicating it in plot to kill Trump". Voice of America (kwa Kiingereza). 2024-07-17. Iliwekwa mnamo 2024-07-19.
- ↑ 36.0 36.1 Willis, Haley; Toler, Aric; Fahrenthold, David A.; Goldman, Adam (2024-07-28), "Gunman at Trump Rally Was Often a Step Ahead of the Secret Service", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2024-07-31
- ↑ 37.0 37.1 Geoff Earle (2024-07-14). "'Staged' trends online as Trump trolls push shooting conspiracies". Mail Online. Iliwekwa mnamo 2024-08-03.