Jamila Abbas
Jamila Abbas ni mwanasayansi wa kompyuta, mhandisi wa programu za kompyuta, mfanyabiashara na mjasiriamali nchini Kenya.[1]Yeye ni mwanzilishi mwenza na Afisa mtendaji mkuu wa MFarm Kenya Limited, shirika linalojikita kwenye intaneti ambalo linawasaidia wakulima kupata zana bora zaidi za kilimo, mbegu, kuweza kupata ripoti za hali ya hewa na taarifa za soko.[2] Alishiriki kuanzisha mradi wa M-Farm mwaka 2010.[1]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Jamila alizaliwa nchini Kenya na alisoma shule za eneo hilo kwa elimu yake ya kabla ya chuo kikuu, alihudhuria Chuo Kikuu cha Strathmore na kuhitimu kwa shahada ya sayansi katika Uhandisi wa programu.[3]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuhitimu kwake kutoka Chuo Kikuu cha Strathmore, Jamila aliajiriwa na Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu ya Kenya (Kenya Medical Research Institute)(KEMRI). Pia akawa mwanachama wa iHub, jumuiya ya kiteknolojia, ambapo mafundi hukusanyika ili kubadilishana mawazo. Huko, aliunganishwa tena na Susan Oguya, rafiki yake kutoka chuo kikuu. Mnamo Septemba 2010, Jamila na Susan waliamua kufanya jambo kuhusu hali ngumu ya wakulima wadogo wa Kenya, kwa kutumia teknolojia.[4]
Wanawake hao wawili, pia walijiunga na AkiraChix, jukwaa lingine la wanawake wanaopenda masuala ya teknolojia ya habari. Huko, walikutana na wanafunzi wengine watatu wa Chuo Kikuu cha Strathmore, Linda Omwenga, Lillian Nduati, na Catherine Kiguru. Watano hao waliamua kuingia IPO48, shindano la uundaji wa programu. Tukio hilo, lilihusisha washindani 100, lililoandaliwa katika timu kumi na saba. Lengo lilikuwa kutengeneza programu ya kompyuta, ambayo inaweza kubadilishwa kuwa biashara inayoweza kuuzwa, yote hayo yafanyike ndani ya masaa 48.[4]
Shindano hilo liliandaliwa na HumanIPO, kutoka Estonia. Mnamo Novemba 2011, wanawake hao watano walishinda shindano, kwa kutumia programu yao ya M-Farm, ambayo inawaunganisha wakulima na wauzaji wa mazao ya kilimo, vyama vya ushirika na kuwawezesha kupata bei za sasa za soko kwa ajili ya mazao yao. Wanawake hao watano pia walishinda zawadi ya juu ya shilingi milioni moja za Kenya (takriban dola za Marekani 10,000)[4]
Kundi hilo lilitumia pesa zao za zawadi kuijumuisha M-Farm Kenya Limited, huku Jamila Abbas akiwa Mkurugenzi Mtendaji, na Susan Oguya akiwa Afisa Mkuu wa Operesheni. Linda Omwenga na Catherine Kiguru walikuwa maafisa wa masoko na Lillian Nduati alikuwa afisa mahusiano ya umma.[4]
Abbas wakati huo huo anahudumu kama mkurugenzi wa nchi wa New Vision Foundation,[2] shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu Minneapolis.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 AGRA News (24 Mei 2018). "Jamila Abass: The queen of African Agritech Industry". Westlands, Nairobi: Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-08. Iliwekwa mnamo 8 Mei 2019.
{{cite web}}: More than one of|accessdate=na|access-date=specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 NVO (5 Februari 2017). "Jamila Abbas, tech entrepreneur, to direct New Vision Foundation". New Vision Organization (NVO). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-26. Iliwekwa mnamo 20 Desemba 2017.
{{cite web}}: More than one of|accessdate=na|access-date=specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Makeni, John (7 Januari 2011). "Girls who created social network for farmers". Daily Nation. Nairobi. Iliwekwa mnamo 20 Desemba 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 5 "Girls who created social network for farmers". Daily Nation (kwa Kiingereza). 2020-07-03. Iliwekwa mnamo 2026-02-15.