Isaac Asimov
Isaac Asimov | |
---|---|
Born | mnamo 2 Januari 1920 Petrovichi, Smolensk Oblast, Urusi |
Died | 6 Aprili 1992 Brooklyn, New York City, Marekani |
Occupation | Mwandishi, profesa wa biokemia |
Citizenship | Urusi (utotoni), Marekani |
Education |
|
Alma mater | Chuo Kikuu cha Columbia |
Genres | Bunilizi ya kisayansi, mystery |
Subjects | sayansi, masimulizi, |
Literary movement | Golden Age of Science Fiction |
Spouse(s) |
|
Children | 2 |
Signature |
Isaac Asimov (mnamo 2 Januari 1920 - 6 Aprili 1992) alikuwa mwandishi wa bunilizi ya kisayansi nchini Marekani. Alikuwa pia mtaalamu wa biokemia mwenye PhD kutoka
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Asimov alizaliwa huko Petrovichi, Smolensk, Urusi katika familia ya Kiyahudi. Tarehe ya kuzaliwa haijulikani, ilitokea kati ya 4 Oktoba 1919 na 2 Januari 1920. Alisheherekea sikukuu yake kwenye 2 Januari. Wazazi walihama Marekani pamoja naye alipokuwa na umri wa miaka 3. Alijifunza lugha za Kiyiddish na Kiingereza tangu utotoni.
Alisoma kemia kwenye Chuo Kikuu cha Columbia akahitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 1941 akaendelea kupokea digrii ya uzamivu (PhD) mnamo 1948. Wakati huohuo aliandika pia masimulizi na vitabu. Tangu 1951 alikuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Boston ilhali aliendelea kuandika.
Baada ya mafanikio ya kitabu chake The Naked Sun (1957) aliacha kazi ya kisayansi akaendelea kutunga vitabu vyake.
Aliandika vitabu vingi, hasa masimulizi na riwaya juu ya ustaarabu ujao ambako watu huishi pamoja na roboti yaani mashine zenye uwezo wa kufikiri zinazopewa maumbile ya kufanana na binadamu.
Asimov alitunga pia vitabu vinavyoeleza sayansi kwa watu waskio wataalamu alikuwa mshauri wa kisayansi kwa filamu za Star Trek zilizotengenezwa kwa runinga.
Maandishi
[hariri | hariri chanzo]Vitabu vya Asimov's vilivyokuwa mashuhuri zaidi vilikuwa vitabu vya mfululizo wa Foundation series. Aliandika pia Galactic Empire na Robot Series. Kwa jumla alitunga au alihariri zaidi ya vitabu 500 akaandika barua 90,000 letters. Pamoja na bunilizi ya kisayansi aliandika pia kuhusu sayansi yenyewe, historia, Biblia, fasihi na
Maandishi mengi ya mapema ya Asimov yalikuwa hadithi fupi zilizochapishwa katika majarida na daftari za hadithi za bei rahisi. Miaka baadaye, yalikusanywa na kuchapishwa tena kama makusanyo. Mikusanyiko inayojulikana ni pamoja na I, Robot, The Rest of the Robots, Earth is Room Enough na The Early Asimov.
Orodha ya Asimov
[hariri | hariri chanzo]Asimov alitunga orodha ya vitabu vyake 15, akishauri visomwe kwa utaratibu huu:
- I, Robot (1950). baadaye The Complete Robot (1982).
- Caves of Steel (1954).
- The Naked Sun (1957).
- The Robots of Dawn (1983).
- Robots and Empire (1985).
- The Currents of Space (1952).
- The Stars, Like Dust (1951).
- Pebble in the Sky (1950).
- Prelude to Foundation (1988).
- Forward the Foundation (1993).
- Foundation (1951).
- Foundation and Empire (1952).
- Second Foundation (1953).
- Foundation's Edge (1982).
- Foundation and Earth (1986).
1-5 ni vitabu vya 'Roboti'; 6-8 ni vitabu vya 'Galacticos Empire'; 9-15 ni vitabu vya mfululizo wa Foundation . [1]
Riwaya za Asimov zimeathiri bunilizi ya kiayansi kwenye runinga na sinema. Hasa 'Three Laws of Robotics' (kanuni tatu za uroboti) zilichangia kwenye majadiliano ya kimataifa kuhusu teknolojia hiyo.
- Roboti haiwezi kumdhuru mwanadamu au, kwa kutotenda, kumruhusu mwanadamu aje ajeruhi.
- Roboti inapaswa kutii maagizo yoyote ambayo wanadamu wamepewa, isipokuwa pale ambapo maagizo hayo yatapingana na Sheria ya Kwanza.
- Roboti lazima ilinde uwepo wake maadamu ulinzi huo haugongani na Sheria ya Kwanza au ya Pili.
Imani
[hariri | hariri chanzo]Ingawa alizaliwa katika familia ya Kiyahudi, Asimov alijiita kafiri anayekana Mungu:
- "Mimi ni kafiri kabisa. Ilinichukua muda mrefu kusema hiyo. Nimekuwa mtu asiyeamini Mungu kwa miaka mingi, lakini kwa namna fulani ... ilikuwa afadhali kusema ni humanisti au mtu asiyejua kama Mungu yupo au la." [2]
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Alipofanyiwa upasuaji wa moyo mnamo 1983, alipokea damu iliyoambukizwa VVU. Alipata UKIMWI, akafa kutokana na athari za hali ya kiafya mnamo 1992.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 15-Book reading order as suggested by Asimov Archived 16 Mei 2006 at the Wayback Machine. From "Author's Note" of Prelude to Foundation Doubleday 1988 hardcover edition.
- ↑ Free Inquiry (Spring 1982). Wikiquote
- ↑ "Letter from Janet Asimov". Locus Online. Locus Publications. 4 Aprili 2002. Iliwekwa mnamo 2012-12-04.
{{cite web}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Angalia mengine kuhusu Isaac Asimov kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
- Asimov Online, a vast repository of information about Asimov, maintained by Asimov enthusiast Edward Seiler
- Jenkins' Spoiler-Laden Guide to Isaac Asimov, reviews of all of Asimov's books
- Annotated Bibliography of Asimov's work by Asimov enthusiast Steven Cooper, claims the most complete bibliography in existence [1]
- Isaac Asimov at the Internet Movie Database}
- Guardian Books "Author Page", with profile and links to further articles.
- Frederik Pohl kuhusu Asimov
- Isaac Asimov Memorial Debates, with videos, at the Hayden Planetarium
- Information about Asimov's ancestors at byrnefamily.net (retrieved February 24, 2019)
- 15-Book Reading Order as Suggested by Asimov From "Author's Note" of Prelude to Foundation Doubleday 1988 hardcover edition
- Works by Isaac Asimov katika Project Gutenberg
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Isaac Asimov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |