Ilangala
Ilangala ni kata ya Wilaya ya Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Msimbo wa posta ni 33615.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 30,329 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 38,008 waishio humo.[2]
Tarafa ya Ilangala
[hariri | hariri chanzo]Ilangala ni pia jina la tarafa, ambayo ni miongoni mwa tarafa nne za Wilaya ya Ukerewe. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, tarafa hiyo ilikuwa na wakazi wapatao 139,329 waishio humo.
Tarafa ya Ilangala inaundwa na kata saba ambazo ni: Ilangala, Kakukuru, Namilembe, Muriti, Nduruma, Igalla na Bwiro.
Tarafa ya Ilangala ina jumla ya vijiji 30 na vitongoji 197. Tarafa hii pia ina visiwa zaidi ya 18 vinavyokaliwa na watu.
Shughuli kubwa za wananchi ni kilimo, ufugaji na kwa sehemu kubwa ni uvuvi.
Makao makuu ya Tarafa ni Muriti.
Taasisi za Umma zilizopo katika tarafa ya Ilangala ni pamoja na:
Shamba la miti la Rubya (TFS-Rubya).
Ulinzi na Usalama: tarafa ina jumla ya vituo viwili vya Polisi (Muriti na Selema) na kila kijiji kinao Askari wa Jeshi la Akiba kwa ajili ya kudumisha Ulinzi na Usalama katika maeneo hayo.
Elimu: kila kata inayo shule ya Sekondari na baadhi ya kata zina Sekondari zaidi ya moja, kwa mfano Muriti na Nduruma. Kila kijiji kina shule ya msingi na baadhi ya vijiji vina shule zaidi ya moja. Elimu katika visiwa inatolewa.
Afya: kila kata inayo huduma ya afya kwa ngazi ya zahanati, pia kuna vituo viwili vya afya (Igala na Muriti).
Haki: tarafa inayo Mahakama ya Mwanzo moja.
Huduma nyinginezo: tarafa inazo huduma zote muhimu kama vile mawasiliano, maji n.k.
Utalii: tarafa ya Ilangala inavyo vivutio vya utalii kama vile 1. Makumbusho ya Handebezo yaliyopo kijiji cha Halwego, kata ya Nduruma 2. Ufukwe wa mchanga mweupe wa Rubya yaani Rubya beach 3. Ngoma na vyakula vya asili kama vile kitoweo cha samaki aina ya ngere.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Ukerewe - Mkoa wa Mwanza - Tanzania | ||
---|---|---|
Bukanda • Bukiko • Bukindo • Bukongo • Bukungu • Bwiro • Bwisya • Igalla • Ilangala • Irugwa • Kagera • Kagunguli • Kakerege • Kakukuru • Mukituntu • Muriti • Murutunguru • Nakatunguru • Namagondo • Namilembe • Nansio • Nduruma • Ngoma • Nkilizya • Nyamanga |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ilangala kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |