Nenda kwa yaliyomo

Ikulu ya Manhyia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ikulu ya Manhiya,upande wa mbele, jengo la kwanza lilikamilika mwaka 1925.

Ikulu ya Manhyia ni makazi rasmi ya Asantehene, kiongozi wa Waashanti.[1].

Ikulu hiyo inapatikana Kumasi, mji mkuu wa ufalme wa Ashanti katika mkoa wa Ashanti; ndiyo ikulu ya kwanza, ila kwa sasa ni makumbusho yanayopatikana katika nchi ya Ghana.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ikulu hii ilijengwa na Waingereza mwaka 1925[2] baada ya vita vya Ashanti mwaka 1874. Hii ni baada ya Waingereza kuharibu jengo la asili la Waashanti. Waingereza walisema walivutiwa na muonekano wa jengo hilo na jinsi lilivyopangika ikiwemo safu yake ya vitabu vya lugha mbalimbali, ila jengo liliharibiwa kwa mabomu [3] .[4]

Asantehene Nana, baada ya kurudi kutoka uhamishoni kwenye visiwa vya Shelisheli, alikabidhiwa nyumba hiyo ikawa makazi yake rasmi, hii ni kwa sababu ya nyumba yake kuharibiwa mara ya kwanza vita vilipopiganwa kati ya Waingereza na jamii ya Waashanti. Chanzo cha vita hivyo kilikuwa kwamba viongozi wa Ashanti waligomea kutoa dhahabu kwa Waingereza Prempeh I alikubaliana na matakwa ya Waingereza baada ya kulipwa gharama za ujenzi wa jengo la kwanza la wafalme wawili waliishi katika jengo hili.

Ikulu ya zamani ilibadilishwa kuwa makumbusho mwaka 1995 baada ya kujengwa kwa ikulu mpya, Opoku Ware II alikuwa wa kwanza kuishi katika ikulu mpya hadi alipofariki mwaka 1999. Hadi sasa makazi haya yanatumika na Osei Tutu II.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Manhyia Palace". Ghana Nation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-16. Iliwekwa mnamo 9 Mei 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Manhyia Palace Museum". lonelyplanet.com. Iliwekwa mnamo 9 Mei 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Lloyd (1964), pp. 172–174, 175
  4. Raugh, Harold E. (2004). The Victorians at War, 1815–1914: an Encyclopedia of British Military History. ABC-CLIO.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ikulu ya Manhyia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.