Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Tanzania
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (kwa Kiingereza: Tanzania National Archives) ni kitengo cha serikali kinachotunza kumbukumbu ya nyaraka za Tanzania. Kama kila taasisi ya nyaraka inatunza faili na ushuhuda mwingine wa kazi ya idara za serikali zilizopita ambazo hazihitajiki tena katika kazi ya kiutawala ya kila siku.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Faili za zamani zaidi kwenye nyaraka zinatokana na utawala wa kikoloni wa Kijerumani. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilivamiwa na Uingereza iliyochukua utawala juu ya maeneo ya Tanganyika. Wakati afisa mmoja Mwingereza alipopitilia karatasi kwenye ofisi za Wajerumani, alikuta amri ya kisiri iliyotolewa mwaka 1916, kabla ya uvamizi wa Dar es Salaam na Waingereza. Amri hiyo ya gavana Heinrich Schnee iliagiza uhamisho wa hati muhimu na kuzificha Tabora kwa kuzizika ardhini.
Mnamo 1921 serikali ya Ujerumani ilikubali kutuma wawakilishi wawili kusaidia serikali ya Uingereza kupata mafaili hayo[1].
Nyaraka hizo zilikuwa msingi wa jalada za Kijerumani katika ofisi ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. [2]
Kwenye Juni ya mwaka wa 1963, baada ya uhuru, serikali mpya ya Tanganyika huru iliomba usaidizi wa UNESCO kumtafuta mtaalamu atakayeanzisha utaratibu wa kuteua mafaili yanayofaa kuhifadhiwa na kuyapanga kwa utaratibu.
Mkurugenzi huyo wa kwanza alikuwa Michael Cook kutoka Uingereza. [3] Alianzisha Idara ya Nyaraka kama ofisi ya serikali. [4] Mbali na maslahi ya kihistoria, nyaraka hizo pia zilikuwa vyanzo muhimu vya kuamua haki za mali au wakati wa kupanga miradi ya ujenzi. [5]
Kwa Amri Nambari 7 ya Rais wa Desemba 1962, Idara ya Nyaraka (Kiing. Records and Archives Management Division) ilikuwa idara ya Wizara ya Utamaduni wa Kitaifa na Vijana. Jalada zilitunzwa mwanzoni kwenye chumba cha chini cha jengo la serikali kwenye bandari ya Dar es Salaam. [6] Michael Cook alijaribu kwanza kutafuta na kukusanya mafaili ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye dari za ofisi za mikoa na wilaya nchini. [7] Alitunga pia sheria ya kwanza ya kumbukumbu na nyaraka ya Tanzania. [8]
Mwaka 1999 idara ilihamishwa kwenda Ofisi ya Rais[9]. Sheria mpya ya mwaka 2002 (Records and Archives Management Act. No.3 of 2002) ilipanusha mamlaka ya idara hiyo inayoratibu sasa utunzwaji wa jalada zote za serikali.
Mnamo Oktoba 1964 idara ilihamia kwenye jengo la zamani la kibiashara katikati mwa jiji, lililokuwa bila kiyoyozi. [10] Mnamo 1984 idara ilipewa majengo yaliyojengwa kwa matumizi yake. [11]
Kumbukumbu na nyaraka
[hariri | hariri chanzo]Jalada kwa lugha ya Kijerumani
[hariri | hariri chanzo]Kuna mafaili zaidi ya 8,000 kutoka kwa utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa kipindi cha 1890-1918. [12] Orodha za jalada zinapatikana. Zimetambuliwa kama Urithi wa Hati za Dunia na UNESCO tangu 1997. [13]
Umiliki wa jalada za Kijerumani mwanzoni ulileta shida maana hakukuwa na mtu yeyote katika idara aliyezungumza Kijerumani. Hapa ilianza ushirikiano na mamlaka ya nyaraka katika Ujerumani ya Magharibi inayoendelea hadi leo na Mamlaka ya Nyaraka za Ujerumani (Bundesarchiv). [14] [15]
Katika muktadha huo, Eckhard Franz alifanya kazi mara mbili kwa kipindi kirefu mnamo 1967 na 1969 katika Jumba la kumbukumbu la Kitaifa [16], kama vile mfanyakazi mwingine kutoka Jumba la kumbukumbu la Jimbo la Marburg. Walipanga akiba na kuzipiga picha. [17] Wanahistoria wa Ujerumani walitumia fursa hiyo na kutathmini nyaraka. [18] Mradi huo ulichukuliwa na Jalada la Shirikisho mnamo 1976. [19]
Jalada lingine
[hariri | hariri chanzo]Nyaraka za Kitaifa za Tanzania [20]:
- Jalada zaidi za 30,000 za Utawala wa Kiingereza (Ofisi ya Katibu Mkuu) kutoka 1919 hadi 1960.
- Nyaraka za zamani za tawala za mikoa na wilaya. Nyaraka hizi zote zimepangwa katika Hifadhi ya Kitaifa kulingana na asili na utaratibu wa asili. Kuna orodha 12 za kutafuta faili za tawala za mkoa na 114 kwa faili za wilaya.
- Nyaraka kutoka kwa wizara za Tanzania, mamlaka, mikoa, wilaya na mashirika ya umma.
- kumbukumbu za misioni na makanisa na nyaraka za kibinafsi kutoka miaka ya 1885-1980.
- mkusanyiko mdogo wa kumbukumbu za kibinafsi, mfano kutoka Universities Mission to Central Africa (UMCA) na kutoka kwa watu kama Shaaban Robert, Saadan Kandoro au Kanyama Chiume.
- Magazeti.
- Gazeti rasmi kutoka 1919 hadi leo.
- Mkusanyo wa ramani na mipango kutoka enzi za ukoloni wa Wajerumani na Waingereza hadi kipindi cha baada ya uhuru.
- Picha kutoka nyakati za Wajerumani na Waingereza na wakati baada ya uhuru.
- Stempu za posta 1963-2000.
- maktaba inayohusiana na historia ya Tanzania.
Fasihi
[hariri | hariri chanzo]- Michael Cook: Meine Tätigkeit in Tansania. Ein Zeitzeugenbericht. In: Archivnachrichten aus Hessen 19/2 (2019), S, 72–75.
- Philip Haas: Deutsche Akten Afrikas. Erschließung und Verfilmung von Kolonialakten durch die Archivschule Marburg und das Bundesarchiv. In: Archivnachrichten aus Hessen 19/2 (2019), S, 65–68.
- Leander Schneider: Tanzania National Archives. History in Africa. 30 (2003), S. 447–454.
- Marcia Wright: The Tanganyika Archives Ilihifadhiwa 24 Februari 2020 kwenye Wayback Machine.. In: American Archivist. 28 (1965), S. 511ff.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyara za Taifa Tanzania
- Chuo Kikuu cha Potsdam : Archivführer Kolonialzeit (Mwongozo wa Nyaraka kwa Historia ya Kikoloni ya Ujerumani)
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://web.archive.org/web/20160716045653/http://www.utumishi.go.tz/archives/archives/index.php?option=com_content&view=article&id=10:history&catid=1:about-us&Itemid=2
- ↑ The United Republic of Tanzania. Records and Archives Management Division Ilihifadhiwa 16 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine.: about us.
- ↑ Haas, S. 65; angalia pia taarifa: Cook: Meine Tätigkeit. (Kijer.)
- ↑ The United Republic of Tanzania. Records and Archives Management Division Ilihifadhiwa 16 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine.: about us.
- ↑ Haas, S. 65.
- ↑ Cook: Meine Tätigkeit, S. 74.
- ↑ Cook: Meine Tätigkeit, S. 74.
- ↑ Cook: Meine Tätigkeit, S. 75.
- ↑ https://www.nyaraka.go.tz/pages/history-legal-mandate Historia / Mamlaka ya Kisheria
- ↑ Cook: Meine Tätigkeit, S. 74.
- ↑ The United Republic of Tanzania. Records and Archives Management Division Ilihifadhiwa 16 Septemba 2016 kwenye Wayback Machine.: about us.
- ↑ The United Republic of Tanzania. Records and Archives Management Division: Archival Holdings.
- ↑ UNESCO: German Records of the National Archives.
- ↑ Cook: Meine Tätigkeit, S. 73.
- ↑ Haas, S. 66f.
- ↑ Vgl. dazu: Birgit Franz: Afrikanische Erinnerungen. In: Archivnachrichten aus Hessen 19/2 (2019), S. 69–71.
- ↑ Haas, S. 65-66
- ↑ Detlef Bald: Deutsch-Ostafrika 1900–1914. Eine Studie über Verwaltung, Wirtschaft und Interessengruppen = Afrika-Studien 54. Diss. Albert-Ludwigs-Universität Freiburg. Weltforum-Verlag, München 1970. ISBN 3-8039-0038-7 (Haas, S. 66).
- ↑ Haas, S. 66.
- ↑ The United Republic of Tanzania. Records and Archives Management Division: Archival Holdings.