Huduma ya Polisi wa Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Polisi wa kitengo cha GSU.

Huduma ya  Polisi wa Kenya (kwa Kiingereza: Kenya Police Service) ndiyo shirika lenye nguvu za katiba za kudumisha ufuatiliaji wa sheria na utaratibu wa umma. Huduma imegawanywa katika kanda, kaunti hadi Polisi wa Tarafa, makao makuu yakiwa katika vituo vya polisi. Wote huripoti katika Makao Makuu ya Kitaifa ya Polisi. Chuo cha Polisi wa Kenya hutawaliwa kutoka makao makuu. Polisi wa Utawala huongozwa tofauti na polisi wengine.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Huduma ya sasa ilianzishwa kama jeshi la polisi la wakoloni Waingereza mwaka 1907. Kutoka mwaka 1887 hadi mwaka 1902, huduma ya polisi ilikuwa inatolewa na Kampuni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Baada ya mwaka 1902, Reli ya Kenya-Uganda ilianzisha vitengo vyake vya polisi.[2]

Kufuatia uhuru wa Kenya, maafisa kutoka Uingereza walibadilishwa kwa Wakenya.

Muundo uliopo[hariri | hariri chanzo]

Huduma ya sasa ina vikosi vitatu ambavyo huripoti kwa Mkaguzi Mkuu wa Polisi, na ni idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa,[3] ambayo ni wizara katika Ofisi ya Rais.

Kila kaunti inaongozwa na Afisa wa Polisi wa Mkoa (PPO); kila mkoa umegawanywa katika tarafa ikiongozwa na Afisa Kiongozi wa Tarafa ya Polisi (OCPD) ambaye kwa kawaida yuko katika cheo cha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP). Tarafa za polisi zimegawanywa katika vituo vya polisi vikiongozwa na Afisa Kiongozi wa Kituo cha Polisi (OCS). Makao Makuu ya Kitaifa ya Polisi wa Kenya yako katika Vigilance House, Harambee Avenue , Nairobi. Mkaguzi mkuu ana wajibu wa kiutawala na wa kushughulikia masuala yoyote yanayogusia wafanyakazi. 

Polisi wa Kenya wana vitengo vifuatavyo[4]:

 • Kitengo cha Polisi wa kuzuia ghasia (GSU)
 • Kitengo cha Polisi wa Mifugo
 • Kitengo cha Polisi wa Kusindikiza Rais
 • Kitengo cha Polisi wenye Mbwa
 • Idara ya Polisi wa Trafiki
 • Kitengo cha Polisi wa Viwanja vya Ndege
 • Kitengo cha Polisi wa Reli
 • Polisi Wanahewa
 • Kitengo cha Polisi wa Utalii
 • Kitengo cha Polisi wa Wanadiplomasia
 • Kitengo cha Polisi wa Baharini
 • Kitengo cha Kitaifa cha Majanga

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. (2010) Crime and Development in Kenya.
 2. https://www.academia.edu/4406247/History_of_the_Police_in_Kenya_1885-1960
 3. Kenya Police. Ministry of Interior and Coordination of National Government.
 4. "Huduma ya Polisi wa Kenya", kenyapolice.go.ke, ilipatikana 20-03-2018.