Nenda kwa yaliyomo

Houari Manar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Houari Manar ( Kiarabu : هواري منار; ‎ Disemba, 1981 - 7 Januari, 2019) alikuwa mwimbaji wa muziki wa raï nchini Algeria ambaye alikuwa maarufu katika nchi yake na pia nchi jirani kama vile Maghreb, Mediterania, na Ufaransa[1] .

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Houari Manar alizaliwa Houari El Madani huko Oran katika familia yenye kaka na dada kumi na wawili. Mama yake alikuwa mwimbaji maarufu wa meddahate , mwigizaji wa muziki wa kitamaduni kwenye sherehe na harusi. Ndugu zake wawili, Cheb Massaro na Cheb Larbi, pia ni waimbaji wa muziki wa raï. Familia iyake ilihamia Marseille, Ufaransa, akiwa na umri wa miaka minne. [2] Katika ujana wake, alitiwa moyo, na waimbaji kama vile Celine Dion, Mariah Carey, na Francis Cabrel . [2]

Mnamo 2003, Manar alirudi Algeria kuanza kazi yake kama mwimbaji wa muziki wa raï, aina ya muziki wa kitamaduni wa Algeria ambao ulianzia miaka ya 1920. [3] Alirekodi nyimbo mbili zilizofaulu, ambazo ni "Cha dani bent nass" na "Kima ndirlek ma terdhach" akiwa chini ya rekodi lebo ya Edition Saint Crépain. Mnamo 2006, alirekodi albamu yake ya kwanza Aâchkek mon traitement na Cheb Kader. Albamu hii ilikuwa ni mchanganyiko wa muziki wa raï na muziki wa kisasa wa pop . [4] [5]

  1. "Houari Manar". Making Queer History (kwa Kiingereza (Canada)). Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  2. 2.0 2.1 Métaoui, Fayçal (9 Januari 2019). "Houari Manar, la voix festive et libre du raï algérien, s'éteint : "Il était l'ami des pauvres"" (kwa French). Iliwekwa mnamo 10 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
  3. "An Introduction to Rai Music". ThoughtCo. ThoughtCo. 2 Mei 2017. Iliwekwa mnamo 7 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "سبب وفاة هواري منار وآخر ظهور له" (kwa Arabic). 10 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 9 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
  5. Lotto Persto, Sofie (8 Januari 2019). "Houari Manar: LGBT fans mourn Algerian singer's sudden death". Iliwekwa mnamo 9 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Houari Manar kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.