Hippokrates

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hippocrates

Hippokrates (Kigiriki Ἱπποκράτης; * mnamo 460 KK kisiwani Kos; † mnamo 370 KK mjini Larisa (Ugiriki)) alikuwa mganga mashuhuri wa Ugiriki ya Kale. Hadi leo waganga hufuata kiapo kinachosemekana kilitungwa na Hippokrates.

Hippokrates huitwa "baba wa uganga". Anafahamika kwa mtindo wake wa kuangalia magonjwa uliokuwa mpya wakati ule. Hakuamini tena ya kwamba ugonjwa wasababishwa na mapepo, uchawi au kwa kumroga mtu. Alifanya utafiti kila mgonjwa akifundisha magonjwa husababishwa na matatizo ndani ya mwili. Hakuelewa bado ya kwamba kuna vijidudu vinavyosababisha magonjwa. Hata hivyo alikuwa na maarifa mengi inayokumbukwa na madaktari hadi leo.

Kati ya mawazo yake ya kudumu ni masharti kwa kazi ya daktari yaliyomo katika kiapo cha Hippokrates:

  • daktari anapaswa kutunza siri ya wagonjwa haruhusiwi kuongea na mtu mwingine juu ya hali yake.
  • daktari anapaswa kutunza maisha hatakiwi kufanya lolote linaloleta hasara