Nenda kwa yaliyomo

Hippokrates

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hipokrate)
Hipokrate.

Hipokrate (kwa Kigiriki Ἱπποκράτης; kisiwani Kos, mnamo 460 KK; Larisa, Ugiriki, mnamo 370 KK) alikuwa mganga mashuhuri wa Ugiriki ya Kale. Hadi leo waganga hufuata kiapo kinachosemekana kilitungwa na Hipokrate.

Hipokrate huitwa "baba wa uganga". Anafahamika kwa mtindo wake wa kuangalia magonjwa uliokuwa mpya wakati ule. Hakuamini tena ya kwamba ugonjwa unasababishwa na pepo, uchawi au ulozi. Alifanya utafiti wa kila mgonjwa, akifundisha magonjwa husababishwa na matatizo ndani ya mwili. Hakuelewa bado ya kwamba kuna vijidudu vinavyosababisha magonjwa. Hata hivyo alikuwa na maarifa mengi yanayokumbukwa na madaktari hadi leo.

Kati ya mawazo yake ya kudumu ni masharti kwa kazi ya daktari yaliyomo katika kiapo cha Hipokrate:

  • daktari anapaswa kutunza siri ya wagonjwa, haruhusiwi kuongea na mtu mwingine juu ya hali yake.
  • daktari anapaswa kutunza uhai, hatakiwi kufanya lolote linaloleta hasara.