Nenda kwa yaliyomo

Himid Mao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Himid Mao Mkami (5 Novemba 1992) ni mchezaji wa kimataifa kutokea nchini Tanzania anayecheza nafasi ya kiungo katika klabu ya Ghazl El Mahalla inayoshiriki ligi kuu ya nchini Misri na Timu ya Taifa ya Tanzania.[1]

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Mao alizaliwa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Baba yake, Mao Mkami, alikua pia mchezaji wa mpira wa miguu na aliiwakilisha Timu ya Taifa ya Tanzania kati ya 1991 na 1995, alifahamika zaidi kwa jina la "Ball Dancer".[2] Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Kiwandani, Turiani, Morogoro, baadae alihamia Karume Dar es Salaam ambapo alisoma mpaka darasa la Sita. Alimaliza elimu yake ya msingi shule ya Msingi Omal Ali Juma iliyopo Magomeni, Dar es Salaam na baadae akajiunga na Shule Ya sekondari Tabata ambapo alihitimu kidato cha nne mwaka 2011.[3]

  1. "Himid Mao Mkami". www.365scores.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-27.
  2. "Mao Mkami : Nditi ananikosha". mtibwasugar.co.tz. 4 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 24 Juni 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ball Dancer JR…Himid Mao Mkami", 28 November 2012. Retrieved on 24 June 2019. (sw) 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Himid Mao kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.