Helsinki
Helsinki | |||
| |||
Majiranukta: 60°10′N 26°56′E / 60.167°N 26.933°E | |||
Nchi | |||
---|---|---|---|
Kaunti | Helsinki | ||
Idadi ya wakazi (2013) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 610 601 | ||
Tovuti: www.hel.fi |
Helsinki (kwa Kiswidi: Helsingfors) ni mji mkuu wa Ufini na pia mji mkubwa nchini. Idadi ya wakazi ni 610,601 (2013) na kuna jumla ya milioni moja katika rundiko la mji.
Jiografia
Helsinki iko kwenye mwambao wa Ghuba ya Ufini ya bahari ya Baltiki; imesambaa mwambaoni wa hori mbalimbali na visiwa vya Ghuba hiyo.
Historia
Manmo 1550 eneo la Helsinki lilikuwa sehemu ya Uswidi na mfalme wa Uswidi Gustav Vasa aliamuru kujengwa kwa mji mpya. Lakini wakati wa utawala wa Uswidi mji ulioitwa kwa Kiswidi "Helsingfors" haukuendela sana.
Tangu mwaka 1809 Ufini ilikuwa chini ya utawala wa Urusi na Kaisari Alexander I wa Urusi aliamuru kuhamisha mji mkuu wa jimbo hili kwenda Helsinki na kujenga mji upya. Tangu wakati ule Helsinki imekua kushinda mji wa Turku uliowahi kuwa mji mkubwa katika Ufini hadi wakati ule.
Tangu mwaka 1917 Helsinki imekua mji mkuu wa nchi mpya ya Ufini.
Viungo vya Nje
Makala hii kuhusu maeneo ya Ufini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Helsinki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |