Hekla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hekla
Hekla ikiwa hai kwenye ramani ya Iceland ya 1585

Hekla ni volkeno iliyopo katika kusini ya Iceland yenye kimo cha mita 1491. Hekla ni volkeno hai inayojulikana kuwa ililipuka zaidi ya mara 20 tangu mnamo mwaka 1104 BK. Kutokana na milipuko hii ya mara kwa mara imeitwa pia "geti ya jahanam".

Umbo la mlima ni ndefu inafanana na safu yenye urefu wa kilomita 40 na kuna kasoko mbalimbali. Milipuko yake ilifunika mara kadhaa uso wa kisiwa cha Iceland, jumla ya majivu ya kivolkeno na fuwawe iliyotemwa na kasoko zake imekadiriwa ni 5 km³ na lava zake kuwa na kiasi cha 8 km³ katika kipind#i cha miaka 1000 iliyopita.

Hekla pamoja na Iceland yote iko juu ya mahali ambako mabamba ya gandunia yanakutana ambao ni bamba la Amerika ya Kaskazini na bamba la Ulaya-Asia na hapo ni sehemu ambako mara kwa mara magma kutoka ndani ya dunia inatoka nje.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: