Hassan Nasrallah
Hassan Nasrallah (31 Agosti 1960 - 27 Septemba 2024) alikuwa kiongozi wa kidini na mwanasiasa ambaye alishika wadhifa wa Ukatibu Mkuu wa Hezbollah (ambacho ni chama cha kisiasa cha Waislamu wa Kishia, kadhalika ni kundi la kijeshi) kuanzia 1992 hadi kuuwawa kwake kisiasa 2024.
Akiwa ni mzaliwa katika familia ya Ki-shi'a mnamo mwaka 1960 kwenye viunga vya mji wa Beirut, Nasrallah alisoma na kuhitimu katika mji wa Tyre, pale alipojiunga kwa muda kwenye Vuguvugu la Amal na baadae kwenda kusoma kwenye seminari ya Kishia huko Baalbek. Baadae alisoma na kufundisha katika shule ya Amal.
Nasrallah alijiunga na Hezbollah ambayo ilianzishwa ili kupambana na uvamizi wa Israeli huko Lebanoni mwaka 1982. Baada ya kupitia kipindi kifupi cha mafunzo ya kidini huko Iran, Nasrallah alirejea Lebanon na kuwa kiongozi wa Hezbollah kumrithi mtangulizi wake, Abbas al-Musawi, ambaye aliuwawa kisiasa kupitia shambulizi la anga lililofanywa na Israeli.[1][2]
Hassan Nasrallah amekuwa kiongozi wa sita katika orodha ya viongozi wa Hezbollah waliouawa na Israeli katika mwaka 2024 pekee. Viongozi wengine waliouawa katika kipindi hicho ni Fu'ad Shukr, Ibrahim Aqil, Ahmad Wehbe, Ibrahim Kobeissi, Mohammad Surour na Nabil Qaouk[3]. Kuanzia Oktoba 29, 2024, nafasi yake imerithiwa rasmi na Ayatollah Naim Qassem.[4]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.aljazeera.com/news/2006/4/10/profile-sayed-hassan-nasrallah
- ↑ https://web.archive.org/web/20160328084825/http://www.cfr.org/lebanon/hezbollah-k-hizbollah-hizbullah/p9155
- ↑ https://apnews.com/article/hezbollah-lebanon-nasrallah-israel-8b2ae56a54d641c6910a79e9e5699824
- ↑ https://www.reuters.com/world/middle-east/hezbollah-elects-naim-qassem-succeed-slain-head-nasrallah-2024-10-29/