Naim Qassem
Naim Qassem | |
Katibu Mkuu wa Hezbollah
| |
Aliingia ofisini 29 October 2024 | |
mtangulizi | Hassan Nasrallah |
---|---|
Naibu Katibu Mkuu wa Hezbollah
| |
Muda wa Utawala 1991 – 29 October 2024 | |
tarehe ya kuzaliwa | 1953 Beirut, Lebanon |
chama | Hezbollah |
ndoa | jina halijatajwa |
watoto | 6 |
Religion | Twelver Shi'ism |
Naim Qassem (kwa Kiarabu نعيم قاسم, alizaliwa Basta Tahta, Beirut, 1953) ni kiongozi wa kidini wa Washia wa Lebanoni ambaye pia ni mwanasiasa aliyehudumu katika nafasi ya Katibu mkuu wa Hezbollah tangia Oktoba 2024.[1]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Qassem alizaliwa katika familia ya Ki-Shia yenye asili ya Kfar Fila.[2][3][4] Alikulia Beirut. Alisomea theolojia na mwalimu wake alikuwa Ayatollah Mohammad Hussein Fadlallah.[3] Alipata shahada ya kwanza ya kemia kwenye Chuo Kikuu cha Lebanoni.[3]
Maisha ya kikazi
[hariri | hariri chanzo]Qassem alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Umoja wa Wanafunzi Waislamu wa Kilebanoni kwenye miaka ya 1970.[4] Alijiunga na Vuguvugu la Amal wakati likiongozwa na Musa al-Sadr.[3][2] Alijitenga na Amal mnamo 1979.[2] Qassem alikuwa kiongozi wa Chama cha Wanazuoni wa Elimu ya Dini ya Kiislamu kuanzia 1974 hadi 1988.[4] Pia alihudumu kama mshauri wa shule za al-Mustafa.[4] Qassem alishiriki katika shughuli za uasisi wa Hezbollah, na mnamo mwaka 1991, akawa naibu Katibu Mkuu wa kundi hilo.[3][5]
Ukatibu Mkuu wa Hezbollah
[hariri | hariri chanzo]Kwa zaidi ya miaka 30, Naim Qassem amekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Hezbollah na mmoja wa viongozi waliotambulika zaidi kwenye kundi hilo. Mnamo Oktoba 29 2024, Qassem anachukua nafasi ya kiongozi wa muda mrefu wa kundi hilo Hassan Nasrallah, ambaye aliuwawa na shambulio la anga la Israeli mjini Beirut mwezi Septemba[1].
Qassem ni kiongozi pekee wa ngazi za juu aliyebaki nje ya orodha ya viongozi wa Hezbollah waliouawa na Israeli. Kuteuliwa kwake kunajiri wakati Hezbollah wako katika mapambano makali na Israeli.[6]
Uongozi mpya wa Hezbollah baada ya Ayatollah Nasrallah ulitarajiwa umwendee Sheikh Hashem Safieddine, lakini siku ya tarehe 22 Oktoba 2024, iliwekwa bayana kuwa ameuwawa kwenye shambulio la anga la Israeli karibu wiki tatu nyuma.
Akijibu juu ya uteuzi huo wa Qassem kupitia mtandao wa kijamii, Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant aliuelezea kuwa ni "uteuzi wa muda" na "si wa kudumu"[6][7]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Hezbollah elects Naim Qassem to succeed slain head Nasrallah". Reuters. 2024-10-29. Iliwekwa mnamo 2024-10-29.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 "Who is Sheikh Naim Qassem, Hezbollah's deputy leader who spoke on Monday?", Reuters, 30 September 2024.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Sayyed Nasrallah re-elected for another term", 5 December 2009.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 Dominique Avon; Anaïs-Trissa Khatchadourian; Jane Marie Todd (10 Septemba 2012). Hezbollah: A History of the "Party of God". Harvard University Press. uk. 210. ISBN 978-0-674-06752-3. Iliwekwa mnamo 14 Aprili 2013 – kutoka books.google.com.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Hizbullah Renews Nasrallah as Head of Shiite Party; Forms A New Shura Council", 20 November 2009.
- ↑ 6.0 6.1 https://www.bbc.com/news/articles/c89vx50g4l5o
- ↑ https://www.washingtonpost.com/world/2024/10/29/hezbollah-new-leader-naim-qassem/