Hezbollah
Mandhari
Hezbollah (kwa Kiarabu: حزب الله , ikimaanisha Chama cha Allah [Mungu]) ni chama cha Waislamu wa dhehebu la Shi'a nchini Lebanoni. Chama hiki kina tawi la masuala ya kiraia na pia tawi la kijeshi. Chama hiki kilianzishwa 16 Februari 1985 na Sheikh Ibrahim al-Amin. Kuanzishwa huku rasmi kulifuatia kutangazwa kwa manifesho ya Hezbollah. Moja ya matamko ndani ya manifesto hii ni tamko la vita dhidi ya Israeli kwa kuivamia na kuikalia nchi ya Lebanoni.
Kutokana na uvamizi huo, Hezbollah iliingia katika kipindi cha mapambano na Israeli hadi mwaka 2000 ambapo Israeli iliondoka katika maeneo iliyokuwa imeyakalia katika upande wa kusini mwa Lebanoni.
Kiongozi wa chama hiki hivi sasa ni Katibu wake mkuu, Sayyed Hassan Nasrallah.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Hezbollah Archived 19 Julai 2006 at the Wayback Machine.
- Luninga ya Hezbollah: Al-Manar TV Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Redio ya Hezbollah: Al-Nour radio Archived 30 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Hezbollah ni akina nani?
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |