Kundi la kijeshi
Kundi la kijeshi ni jeshi lisilo rasmi na wala si sehemu ya jeshi ambalo linatambulika na sheria za nchi husika.[1] Kwa mujibu wa uchunguzi juu ya historia ya makundi haya, wataalam wamebaini kuwa makundi haya yamekuwepo tangia mwaka 1934.[2]
Ingawa kifasili kundi la kijeshi huonekana si jeshi, kwa kawaida huwa sawa na jeshi la askari wa miguu wasio na zana nzito au vikosi maalum kwa mujibu wa nguvu, stadi (kama za uteguaji wa mabomu), mbinu (kama za mapambano ya msituni au kwenye miji), ukali wa mapambano na hata muundo wake wa kamandi.[3]
Kundi la kijeshi linaweza kuingia kwenye mfumo wa jeshi la nchi, likajifunza pamoja nao, au kupata ruhusa ya kutumia zana zao, ingawa wao si wenzao.
Uhalali
[hariri | hariri chanzo]Chini ya Sheria ya Vita, taifa linaweza kulijumuisha kundi la kijeshi au wakala wa kijeshi (kama vile vyombo vya kusimamia utekelezwaji wa sheria) au jeshi binafsi la kujitolea, kwenye jeshi lake la mapambano. Baadhi ya nchi zina katiba zinazokataza uwepo wa makundi ya kijeshi nje ya jeshi la taifa au kutumika nje ya maslahi ya kitaifa.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://oed.com/search?searchType=dictionary&q=paramilitary
- ↑ https://www.oed.com/search/dictionary/?q=paramilitary
- ↑ https://www.pbs.org/newshour/world/wider-conflict-feared-as-sudans-army-and-rival-paramilitary-force-clash-in-capital